Home » » DAAAH HII LAANA GANI HII??!......JAMAA KAMUUA MAMA YAKE

DAAAH HII LAANA GANI HII??!......JAMAA KAMUUA MAMA YAKE



Kijana pichani hapo juu anaetambulika kama Frank Hillary, mwenye umri wa miaka 27 anashikiliwa na police kwa tuhuma za kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake huyo. 
Tukio zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya Chamwino, mkoani hapa na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake. 

HALI HALISI ILIVYOKUWA
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake. “Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza: “Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”
Shuhuda mwingine, Julius Josephat alisema: “Mimi nashindwa kuelewa. Huyu marehemu na mwanaye walikuwa wanapendana sana, wakienda kanisani wanaongozana kama kumbikumbi.
“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa mama yake aliumia mkono kama siku tatu kabla, akawa amefungwa plasta ngumu (POP), nahisi ndiyo maana alishindwa kujiokoa.” 
Naye Maria Maswika ambaye nyumba yake imepakana na ile ya mama Hillary, alieleza: “Leo (Alhamisi),  saa 4 asubuhi nilimsikia huyo mama akipiga kelele za kuomba msada, huku akiingia nyumbani kwangu.

“Nilipotoka chumbani, nilishuhudia kwa macho yangu yule kijana akimpiga shoka mama yake na kumuua palepale. Sababu ya ugomvi wao siielewi. Kwanza nashangaa sana, kwani yule mama wa watu alikuwa anampenda sana mtoto wake.”





Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio...

muuaji akiwekwa chini ya ulinzi................

HILLARY AKAMATWA
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio mapema na kushuhudia wananchi wakimkamata Hillary, kumfunga kamba kabla ya polisi nao kuwasili, kuandika maelezo na kumchukua mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mama yake mzazi.
RPC ANASEMAJE KUHUSU SHERIA?
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile, alisema: “Uchunguzi zaidi wa tukio unaendelea na utakapokamilika, tutamfikisha mtuhumiwa mahakamani.”

                

Habari zaidi check GPL
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger