MTOTO WA MIAKA 10 AFA MAJI WAKATI AKITOKEA KUOKOTA KUNI - MBEYA


Mtoto aliyefahamika kwa jina la Eva Mathias Kankolwe mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Kata ya Kiwira wilayani Rungwe amekufa maji baada ya kutereza katika kivuko cha mto Kiwira wakati akitokea kuokota kuni.

MWANDISHI WETU GREYSON SALUFU AMETUANDALIA TAARIFA IFUATAYO..... Bofya hapo chini kusikiliza habari kamili.

Tuzo ya mwalimu bora duniani yazinduliwa



Mwenyekiti wa Wakfu huo Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.





Baadhi ya walimu jijini Mbeya  wameipokea kwa mtazamo tofauti  juu ya kuzinduliwa kwa tuzo ya mwalimu duniani, atakaye thibitisha kuwa mchango wake kwa jamii umekuwa bora zaidi na kujishindia shilingi bilioni 1 na milioni 650.



KWA HABARI KAMILI INALETWA KWAKO NA GREYSON SALUFU...... Bofya hapa chini kwa habari kamili.

Malaysia:Ndege ilianguka baharini

Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak.


Shirika la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.

Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.
Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.

Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko.

Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.

Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.

Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.

Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.

Chanzo - BBC

Rafiki wa Jackie Cliff athibitisha kuwa ndiye aliyekamatwa na dawa za kulevya China, asema kuna uwezekano akaikwepa adhabu ya kunyongwa.


Hivi karibuni gazeti kubwa nchini China la ‘China Daily’ lilichapisha habari kuhusu kukamatwa kwa msichana mwenye umri wa miaka 28 raia wa Tanzania aliyekutwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 85.


Japokuwa gazeti hilo halikutaja jina la msichana huyo huku picha zikimuonesha akiwa amefunikwa uso na hivyo kutotambulika kirahisi, kiongozi wa kundi la Rockaz, Chief Rocker ambaye yupo nchini China kimasomo amethibitisha kuwa msichana huyo ni Jackie Cliff ambaye pia ni rafiki yake wa karibu.

Chief Rocker ameuambia mtandao wa Bongo 5 kuwa amethibisha kuwa aliyekamatwa ni Jackie Cliff baada ya kuongea na ubalozi wa Tanzania nchini humo.

“Amekamatwa kweli. Nilivyosikia story ni kwamba ametoka Bongo akapita Thailand akaenda Macau, Macau ndio akakamatwa. Mimi nilijua kwa sababu nilipigia simu watu wa ubalozi baada ya kupata taarifa tu mara ya kwanza nikawapigia watu wa ubalozi nikawaambia ‘bana, ndugu yetu amekamatwa sasa nataka kujua process ikoje kama kuna kumuona ama kama kuna chochote. Kuna ubalozi mwingine mdogo uko Hong Kong wao ndio wakanambia mambo yalivyo kwamba alikuwa yupo yeye na watu wengine wawili, Mtanzania na Mnaijeria, yeye ndiye akakamatwa , hawa wengine baada ya kuona wanataka kukamatwa wakakimbia.” Amesema Chief Rocker.

Chief ameeleza kuwa kutokana na sheria za Macau kuwa tofauti na za bara nchini China, Jackie anaweza asihukumiwe kunyongwa kama ilivyo kwa sheria za bara.

“Inategemea, ukikamatwa Mainland China au labda ukakamatwa Macau au kwa Macau na Hong Kong ni kama huko kwetu, ni kama Tanzania na Zanzibar. Kwa hiyo yeye alikokamatwa ni kama yuko Zanzibar, ni ndani ya China lakini inategemea sheria zake sio kali sana.

“Lakini sasa mpaka wajaji kutokana na mzigo ulioubeba. Wengine wanasema miaka mitatu, wengine minne, wengine wanasema wanatoa kama Hong Kong miaka nane, so inategemea akiwasaidia polisi akisema watu aliokuwa akiwapelekea mzigo wako wapi na wakapatikana, I don’t know.” Chief ameuambia mtandao wa Bongo 5.

Chief ameonesha kumuhurumia Jackie kwa maisha atakayokaa jela nchini China kwa kuwa hafahamu Kichina, hivyo itakuwa ngumu sana yeye kuweza kuwasiliana na mahabusu wenzake katika hali ya kawaida (Ku-socialize). 

TAMKO LA RAIS NA AMIRI JESHI MKUU JAKAYA MRISHO KIWETE KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA NA KUUWAWA KWA WANAJESHI SABA WA JWTZ WALIOKUWA WAKILINDA AMANI DARFUR SUDAN.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokuwa wanalinda amani katika eneo la Darfur, Sudan.

Kwa hakika, Rais amesikitishwa sana na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania wamejeruhiwa na waasi wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni mwake kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.

Aidha, Rais Kikwete anaungana na Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia anaungana na Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo waweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Adolf Mwamunynge na familia za wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na waassi.”

Rais Kikwete ameongeza kumwambia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya Watanzania wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea walipokwenda Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao.”

Amesisitiza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa Jeshi letu kwa kupotelewa na wenzao. “

“Aidha, kupitia kwako, natuma salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. 


Wajue kuwa uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za marehemu. Amina”.

Kwa walioumia, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu katika kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.”

Vijana hao waliopoteza maisha yao na walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur kutoka eneo la Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai 13, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

14 Julai, 2013

MISAADA ZAIDI YAENDELEA KUTOLEWA KWA MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI MIAKA MIWILI.

 Christian Mwakapusya Mtanzania anaeishi Marekani  akiwa amembeba mtoto Joshua Joseph baada ya kumtembelea nyumbani kwao Iyunga Jijini Mbeya

 David Mwakapusya ambaye alifuatana na Baba yake akitoa msaada wa nguo kwa mtoto ambaye hakufahamika jina lake kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mtaani hapo.
 Baadhi ya Majirani wa familia ya Joshua wakiwa na nguo walizopewa na Christian Mwakapusya
 Christian Mwakapusya akizungumza na mama mlezi wa mtoto Joshua Joseph Nyumbani kwake Iyunga Jijini Mbeya.

Christian Mwakapusya akizungumza na Amina Mwasankinga aliye simamishwa masomo kwa kisingizio cha ushirikina alipo kutana nae katika Ofisi za Mbeya yetu.
******************

MTANZANIA anayeishi Marekani Christian Mwakapusya aliyeguswa na kitendo alichofanyiwa  mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili kufungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.

Kutokana na kuguswa na tukio hilo Mtanzania huyo amelazimika kumtembelea Nyumbani anakoishia na kujionea hali halisi aliyonayo mtoto huyo kwa sasa.

Akizungumza kwa masikitiko nyumbani kwao eneo la Iyunga Mwakapusya amesema Wazazi wanaofanya vitendo kama hivyo wanapaswa kulaaniwa na kukemewa.

Mwakapusya aliyekuwa amefuatana na Mtoto wake wa Kiume David waliofunga safari kutoka Marekani hadi Mbeya kumwona Mtoto huyo wametoa zawadi mbali mbali zikiwemo Nguo na fedha taslimu alizokabidhiwa Mama mlezi pamoja na Balozi wa Nyumba kumi.

Mhanga wa tukio hilo, Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .

Balozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaakwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.

Wakati huo huo Msamaria mwema huyo kutoka Nchini Marekani pia amezungumza na Mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Amina Mwasankinga ambaye alifukuzwa Shule kwa kisingizio cha Ushirikina.

Aidha amemuahidi kumsaidia ili aweze kumaliza masomo yake huku akilaani vikali kitendo cha Walimu wa Shule ya Hollwood ya Wilayani Mbozi kuamini imani za Kishirikina na kumharibia masomo Mwanafunzi huyo.

VERY SAD NEWS: BINTI AFARIKI DUNIA SAA MOJA KABLA YA HARUSI YAKE..



Marehemu Levina Mmasi akilishwa chakula na aliyetarajia kumuoa, Kasisi Masawe kwenye hafla ya kuagwa kwake  (Send-Off Party) iliyofanyika Jumatano iliyopita. 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Bibi Harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa katika Kanisa la Katoliki la Roma Wilaya Handeni Jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa ya msiba.
Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo.
Msemaji wa familia ya marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Firmin Mrimasha, alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levina ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.
 “Huyu bibi harusi alikuwa ametoka kujifungua, alikuwa na mtoto wa kiume kutokana na ujauzito wa miezi saba, ndipo ghafla Alhamisi akapata homa tukampeleka hospitali alikolazwa na baada ya kupata nafuu, aliruhusiwa Ijumaa.
“Baada ya kuruhusiwa akaanza maandalizi ya harusi na Jumamosi ambayo ndiyo siku ya ndoa yake, alijiandaa lakini ilipofika saa 8.05 akafariki dunia akiwa nyumbani akisubiriwa kwenda kanisani kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifungwe saa 9.00,” alisema Mrimasha.
Alisema, “Inasikitisha sana ila imeshatokea yaani marehemu amefariki saa moja kabla ya ndoa yake na baada ya kifo hicho, mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya mama yake kufariki dunia,” alisema Mrimasha.
Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi hiyo iliyogharimu Sh7.7 milioni, Abdi Kipacha alisema kuwa kwake ni tukio la kwanza kutokea tangu kuzaliwa kwake na kamwe hawezi kulisahau.
“Nilishazipangia kazi kamati za maandalizi, lakini ghafla tukapewa taarifa kuwa bibi harusi amefariki…Hatukuamini, ikabidi niwatangazie wanakamati wenzangu kuwa hakuna tena shughuli, bibi harusi amefariki,” alisema mwenyekiti huyo wa kamati na kuongeza:
“Kitu tulichokuwa tukisubiri ni kuambiwa bibi harusi angefika saa ngapi, lakini ghafla tukapewa taarifa za kifo, ilikuwa ni vigumu kuamini lakini ni kweli imetokea na inasikitisha kwani si jambo la kawaida,” alisema Kipacha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wanandugu ni kuwa marehemu alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Nndawa mkoani Lindi na kwamba alikuwa katika kundi la walimu wa ajira mpya ambayo hadi mauti yanamkuta alikuwa hajapokea hata mshahara wake wa awali.
Akizungumzia hali hiyo, Padri aliyekuwa afungishe ndoa hiyo, Max Sabuni wa kanisa hilo Katoliki Handeni alisema:       “Nimesikitishwa na tukio hili kwa kuwa halikuwahi kunitokea…Kilichobaki ni wanandugu kuwa watulivu kwa kuwa Mungu amechukua kiumbe wake kwa muda alioupanga.”
Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi.
Habari na : mwananchi.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger