Home » » UUWWII MASKINI RAY C

UUWWII MASKINI RAY C

                   
MAMA mzazi wa staa wa Bongo Fleva mwenye skendo ya kugigida madawa ya kulevya, Rehema Chalamila  ‘Ray C’, Magret Mtweve ametoa tamko kali dhidi ya aliyekuwa mpenzi wa mwanae, Isaac Makuto ‘Lord Eyez’ kutotia mguu nyumbani kwake Kunduchi, Dar. Mama Ray C alichimba mkwara huo wakati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mbalimbali Jumatatu iliyopita alipoulizwa kama Ray C amerudi nyumbani kwake baada ya kutoweka kitambo. Mama yake alisema, “Amerudi jana jioni (Jumapili). Nilipomuuliza amesema alikuwa Kariakoo, lakini hataki kuwataja aliokuwa nao wala alichokuwa akikifanya. “Nimekuwa nikizunguka kwenye makanisa mbalimbali kumuombea njia, naona ameanza kuleta matumaini...lakini sitaki kabisa kumsikia mtu anayeitwa Lord Eyez, yeye na wenzake ndiyo waliomsababishia matatizo haya mwanangu,” alisema mama huyo.
                
Pichani juu ni mama mzazi wa Ray C Magret Mtweve, akiwa katika masikitiko makubwa kutokana na hali aliyonayo mwanae hivi sasa, anaomba watu wajitokeze kumsaidia na sio kukaa na kuanza kumbeza mwanae, maskini mama pole sana i know how painful kumuona mtoto wako akiwa katika hali kama hio, very sad kwa kweli, endeleza maombi mama, Mungu yupo atamsaidia tu

Ray C (enzi za uzuri wake) na Lord eyez ambae ndio anatuhumiwa na ndugu wa Ray c kua ndie aliemuharibu binti huyo kwa kumuonyesha mambo ya madawa ya kulevya, wakati huo huo lord eyes amegoma tuhuma hizo na kudai eti alikumkuta Ray c tayari teja tokea zamani , but all in all tuombee Taifa letu Tanzania vijana waache haya mambo ya kuiga Wamarekani na kujiharibia maisha jamani,,,uuwwiiii

Habari na GPL na Mpekuzi
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

3 comments:

Anonymous said...

Daaah huyu mtoto ndio kawa hivi?

Anonymous said...

Maskini kiuno bila mfupa

Anonymous said...

duuh huyu jamaa si ndio naye kawa teja anaiba kwenye magari ya wasanii wenzake?? duuh bongo wasanii wanaisha jamani

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger