Home » » UTALII WA NGONO WAIBUKA TANZANIA

UTALII WA NGONO WAIBUKA TANZANIA



Baadhi ya vivutio hivi ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango na nyumba za kihistoria. Hata hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar. Imebainika kuwa katika utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka 60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.Sugar Mummies image (photo: Nobby Clark)

Uchunguzi huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta mwanamume atakayestarehe naye kingono. Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa kustarehe nao
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, utalii huu umeshamiri nchini, ambapo vijana wa Kitanzania wanaufahamu na kukiri kuwa umewanufaisha na baadhi yao kuwasaidia kupata tiketi za kwenda kuishi Ulaya. Katika Visiwa vya Zanzibar utalii huo unafanyika zaidi katika fukwe za Nungwi, Kiwengwa, Paje, Kendwa, Jambiani na maeneo mengine yaliyopo pembezoni mwa bahari.
Na: Mwananchi..

**** mweeeh MABIG**** 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

2 comments:

Anonymous said...

ha ha ha ha na walikua wanasema wanawake tu kua wanawafata wazungu kumbe wazungu nao wanawafata wanaume wetu Africa? sasa mna hate nini?

Anonymous said...

Wazungu sex kwao ni kuhave fun sio big deal, wabongo ndio mnachukulia big deal...

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger