Marehemu Mariam Khamis enzi za uhai wake
Mamia
ya watu walijitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini
Mariam Khamis maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati
akijifungua. Mariam alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambapo mtoto wake alisalimika.
Mazishi
hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina
mbalimbali wakiwemo wasanii wengine wa muziki wa Taarab.
Miongoni
mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha
Mashauzi, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila, Nyota Waziri, Bi Hindu na
wasanii wenzake wa kundi la TOT.
Mwili wa marehemu Mariam Khamis ukiwa unaelekea makaburini mapema leo
Mamia ya watu walio jitokeza kumsindika dada Mariam kwenye nyumba yake ya milele
Mume wa marehemu Mariam Khamis akiingia ndani ya kaburi tayari kwa kumzika mkewe pembeni yake ni baba mkwe wake
Tayari kwa kupokea mwili wa marehemu pindi uingizwapo ndani ya kaburi
Mwili wa marehemu Maraiam Khamis ukiingizwa ndani ya kaburi
Tayari dada Mariam kashazikwa hapo zoezi la kufukia na mchanga likiendelea
Mwanamuziki wa Taarab Thabit Abdul naye akiiendelea na zoezi la kufukia kaburi la dada Mariam Khamis
Na hii ndio nyumba yake ya mwisho dada Mariam Khamis ambayo ataishi maisha yake yote
Kaburi la marehemu dada Mariam Khamis likiwa katika muonekano ambao tayari lishafukiwa
Mume
wa marehemu Mariam Khamis akiwa haamini kuwa mkewe hayuko naye tena
duniani kiukweli alichokuwa akikiongea hapo pembeni ya kabuli ungekuwepo
wewe rafiki yangu sidhani kama ungeweza kuvumilia lazima ungelia pole
sana kaka HAJI KIJUNGU mbele yake nyuma yetu.
---
Mariam
alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi za uhai wake aliwahi
kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni pamoja na East
Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.
Marehemu
Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya vizuri katika muziki wa
Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.
Picha kwa hisani ya Shakoor Jongo
0 comments:
Post a Comment