Mmoja wa wanufaika wa mradi wa kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula chenye lishe akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya M-pesa atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo hutolewa bila malipo na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.
Akina mama wa kijiji cha Nanguruwe mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe wakijumuika na maofisa wa Vodacom kufurahia simu walizopatiwa zikiwa zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom kuwawezesha kupokea fedha za mradi kwa njia ya M-pesa.
Habari na GPL
0 comments:
Post a Comment