Mshindi wa shindano la kula mende, Edward Archbold (32) amefariki dunia muda mfupi baada ya kula dazeni kadhaa za mende walio hai jijini Miami, Florida Marekani.
Takriban watu 30 walishiriki kwenye shindano hilo la kula mende hai Ijumaa usiku katika dula la mifugo ya mapambo (pets) linalointwa Ben Siegel Reptile Store. Tuzo kwa mshindi ni chatu (Marekani kuna hobby kubwa ya kufuga chatu kwa mapambo) Marehemu Edward ambaye alisema kuwa ameshawahi kula mende nyumbani kwao Dar es Salaam, Tanzania alianza kuumwa muda mfupi baada ya kula wadudu hao, na hatimaye kuanguka katika duka katika duka hilo la mifugo.
Mamlaka inayohusika inasubiri matokeo ya vipimo vya maiti (autopsy) ili kujua chanzo cha kifo cha marehemu Edward. Cha kushangaza ni kwamba hakuna mshindani mwingine yoyote aliyeshiriki kwenye shindano hilo aliyeumwa hata kidogo. Wote wako salama salmini, posili walisema..
Mwanasheria wa mmiliki wa duka hilo lilipofanyika shindano alisema kwamba washiriki wote walisaini makubaliano kwamba wanakubaliana na matokeo yoyote yatakayotokea kutokana na kushiriki shindano hilo, na duka hilo halina jukumu kwa lolote litakalowatokea washindani hao.
Marehemu Edward alikuwa akijulikana kwa mapenzi yake makubwa kwa timu ya Dar Young Africans ya nchini Tanzania
5 comments:
Uwiiiiiiiiii jamani hizi hela zitatuua
Du mashindano mengine bhana ya ajabu kama nini
Duuuuuu mashindano mengine bhana ya ajabu kama nini
Heee kumbe ndugu yetu mwe pole yake sana....kula mende mmh hata niahidiwe dola bilioni siwezi lol hapa nasikiaje kutapika ka mi ndo nimekula!
Ana wazimu huyu, kala mende, mende nao wamemla......duuh
Post a Comment