Home » » JAMAA AFA GHAFLA BAADA YA KUSHINDA SHINDANO LA KULA MENDE WALIO HAI....

JAMAA AFA GHAFLA BAADA YA KUSHINDA SHINDANO LA KULA MENDE WALIO HAI....

edward archbold 0 Mshabiki wa Yanga afariki baada ya kushinda shindano la kula mende hai Marekani

Mshindi wa shindano la kula mende, Edward Archbold (32) amefariki dunia muda mfupi baada ya kula dazeni kadhaa za mende walio hai jijini Miami, Florida Marekani.
Takriban watu 30 walishiriki kwenye shindano hilo la kula mende hai Ijumaa usiku katika dula la mifugo ya mapambo (pets) linalointwa Ben Siegel Reptile Store. Tuzo kwa mshindi ni chatu (Marekani kuna hobby kubwa ya kufuga chatu kwa mapambo) Marehemu Edward ambaye alisema kuwa ameshawahi kula mende nyumbani kwao Dar es Salaam, Tanzania alianza kuumwa muda mfupi baada ya kula wadudu hao, na hatimaye kuanguka katika duka katika duka hilo la mifugo.Victory for short-lived for Edward Archbold who won a roach-eating contest but then mysteriously died shortly after
Mamlaka inayohusika inasubiri matokeo ya vipimo vya maiti (autopsy) ili kujua chanzo cha kifo cha marehemu Edward. Cha kushangaza ni kwamba hakuna mshindani mwingine yoyote aliyeshiriki kwenye shindano hilo aliyeumwa hata kidogo. Wote wako salama salmini, posili walisema..
Mwanasheria wa mmiliki wa duka hilo lilipofanyika shindano alisema kwamba washiriki wote walisaini makubaliano kwamba wanakubaliana na matokeo yoyote yatakayotokea kutokana na kushiriki shindano hilo, na duka hilo halina jukumu kwa lolote litakalowatokea washindani hao.
                                   Archbold, seen here in an undated mugshot, won a snake from the competition    
Marehemu Edward alikuwa akijulikana kwa mapenzi yake makubwa kwa timu ya Dar Young Africans ya nchini Tanzania


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

5 comments:

Anonymous said...

Uwiiiiiiiiii jamani hizi hela zitatuua

Anonymous said...


Du mashindano mengine bhana ya ajabu kama nini

Anonymous said...

Duuuuuu mashindano mengine bhana ya ajabu kama nini

Unknown said...

Heee kumbe ndugu yetu mwe pole yake sana....kula mende mmh hata niahidiwe dola bilioni siwezi lol hapa nasikiaje kutapika ka mi ndo nimekula!

Anonymous said...

Ana wazimu huyu, kala mende, mende nao wamemla......duuh

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger