Kutokana
na viongozi wakuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuzuiwa kuingia
ndani ya bunge wakiwa wamevaa sare za chama, wabunge wa Chadema
wamesusia kuhudhuria kikao cha kupitisha bajeti ya serikali 2013/14
jioni hii ya June 24 2013.
Huo
uamuzi umetangazwa na mnadhimu mkuu wa kambi hiyo Tundu Lissu ambapo
amesema ni kinyume na kanuni ya bunge inayozungumzia mavazi rasmi ya
wabunge wanaume.
Namkariri
Tundu Lissu akisema “Tumeona hatuwezi kushiriki katika shughuli ya
bunge ya leo, tunakwenda kushiriki nini? kufanya uamuzi wa aina gani?
wakati hatujashiriki kwenye mjadala kwenye mjadala kwa sababu ambazo
tumezieleza, hatuwezi tukaingia bungeni kupiga kura kuamua kitu ambacho
hatukukijadili, tumezuiwa kukijadili, tukio la bomu la Olasiti Arusha Mh
Spika aliongoza ujumbe wa Wabunge karibu 30 kwenda kuwapa pole na
kuangalia eneo la tukio, this time watu wameumizwa, watu wamekufa, bunge
halijaahirisha shughuli halitoa mchango hata senti kumi na hakuna hata
wazo la kwenda kuwaona walioumia na waliofiwa”
Kwenye sentensi nyingine, Tundu
Lissu ameonyesha kushangazwa na bunge kuendelea na majadiliano ya
uchumi wa Taifa 2012 na mpango wa maendelea ya Taifa 2013/2014 wakati
kukiwa na tukio la mauaji lililotokea Arusha ambapo watu watatu
walifariki dunia.
Hata
hivyo wakati Chadema wakisusia kikao cha bunge, wabunge wengine walikua
wanatarajia kuipitisha bajeti hiyo ya Serikali ya 2013/14 iliyotenga
zaidi ya Trillioni 18.2 (kwa hisani ya Millardayo.com)
0 comments:
Post a Comment