Mfanyabiashara mmoja katika maduka ya kariakoo alietambulika kwa jina la Shirima, “amejirusha” toka ghorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuangukia gari. Bwana Shirima amekimbizwa hospitali na haijafahamika bado kama amefariki au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo. Chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita, wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima....Tukipa habari zaidi kuhusu tukio hili la kusikitisha tutawajulisha....
0 comments:
Post a Comment