Mama huyu alikutwa sokoni hapo akiuza samaki licha ya eneo alilokuwa akiuzia kuwa na tope na inzi wengi.
Mwandishi wa mtandao huu leo ameshuhudia uchafu uliokithiri katika soko la Buguruni jijini Dar es Salaam ambapo walaji wamesema kama mamlaka husika hazitajali nakufanya usafi, basi kuna tishio kubwa kwa kulipuka magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifanya biashara kwa hali ya shida kutokana na kutiririka kwa maji machafu sokoni hapo
Uchafu uliolundikana katika moja ya kona ya soko hilo ambapo wafanyabiashara wamesema una siku nne sasa bila kuzolewa.
Kutoka: GPL
0 comments:
Post a Comment