HUYU NI MMOJA KATI YA MAJERUHI WENGI WA BOM LILILOLIPUKA LEO KWENYE KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH KULE ARUSHA. AMBAKO BALOZI WA PAPA ALIKUWA AKIHUDHURIA IBAADA YA KUZINDUA PAROKIA KANISANI HAPO.HIVI KWELI NYUMBA ZA IBAADA ZINALIPULIWA KAMA KAMBI ZA WAASI?
EEEEE MUNGU TUSAIDIE....(Picha na maelezo kutoka mdau mmoja huko fb)
Nimepata au niseme nimesoma taarifa za kusikitisha kwamba bomu limelipuka katika kanisa katoliki, parokia mpya ya Olasiti iliyokuwa inazinduliwa leo jijini arusha. Bomu limelipuka wakati waumini wa kanisa la katoliki wakijiandaa na misa ya uzinduzi wa parokia hiyo.
Ambapo mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliojeruhiwa ama kupoteza maisha lakini taarifa za awali zinasema kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa hospitali.
Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama. Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania. Ambapo yupo baada ya kunusurika katika mlipuko huo wa bomu.
Hili ndio kanisa linalosemekana kulipuliwa, daaah yaani mpaka saivi bado nashangaa habari hizi , siamini kama Tanzania tunafanya upumbavu na upuuzi kama huu... kulipuana mpk makanisani jamani? mmmh kweli God has to intervene sasa kwa kweli..it is very sad yaani..
Eneo hili ndio eneo la tukio, panaposemekana kulipuka kwa bomu hilo
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Eneo hili ndio eneo la tukio, panaposemekana kulipuka kwa bomu hilo
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
0 comments:
Post a Comment