Home » » MAMA VIJACHO TZ MASHAKA TELE

MAMA VIJACHO TZ MASHAKA TELE

Vifo vya Mama vijacho(pregnant women) Tanzania ni swala ambalo tumekua tukiliongelea mara kwa mara katika magroup yetu ya wamama katika social Network mbalimbali, ila sasa muda wa kulalamika kati yetu wamama tu umeshaisha, kupitia blog hii, swala hili tutakua tunaliongelea mara kwa mara mpaka ngazi husika walisikie na kama wasipolisikia basi tutaomba wadhamini hata nchi za nje, wamama Tanzania wamekua wakiogopa kuzaa kwa ajili ya huduma mbaya kabisa ya hospital za serikali jamani, wamama wakifika hospital katika hali mbaya walionayo na uchovu mkubwa, wauguzi wamekua wakifanya madudu na wala hawatilii msisitizo na mama wengi wamekua wakipoteza maisha, hapa ninavyosema hivi nina proof ya kupotea kwa mama vijacho wengi tu kwa ajili ya huduma  mbofumbofu Tanzania jamani mlinde mama kijacho Tanzania...lilinde Taifa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

3 comments:

Admin said...

Hii tabia ya madaktari kugoma siku hizi inakuaje kwa mama wajawazito jamani hivi Tanzania kuna nini? Nasikia eti Madactari wameahidi kugoma iwapo Waziri wa afya na katibu wake wasipojiuzulu sasa hapa wanamkomoa waziri wa afya au mama na mtoto mtarajiwa...!!?? mweeh ..naombeni maoni yenu wajameni

doli said...

Yani hii watakomoa wagonjwa na mam vijasho wote,ebu jaribu ku imagine mama kijasho aliyeshikwa na uchungu halafu unafika hospitali unaambiwa kuna mgomo,yani ni kuomba mungu tuu wafikiane muafaka la sivyo itakuwa hatari sana

Doto said...

Uuuwi mi ndo inaniuma balaa hasa wamama ambao haana uwezo waku jilipia kwenye ma hsp ya private jamani inasikitisha sana, ila na serikali yetu nayo imezdi kuwaonea wataalamu jamani mazngra magumu mishahar midogo mwisho mwishoni mama anaathirika sana jamani inaumiza sana.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger