Home »
» Madaktari wasitisha mgomo Tanzania
Madaktari wasitisha mgomo Tanzania
CHAMA cha Madaktari Tanzania (Mat) kimetangaza kusitisha mgomo wa nchi nzima kuanzia jana mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kumheshimu Rais Jakaya Kikwete, huku kikiwatangaza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na naibu wake, Dk Lucy Nkya kuwa maadui namba moja wa sekta ya afya nchini.
Uamuzi huo wa kurejea kazini umekuja siku nne tangu madaktari hao walipoanza mgomo kwa mara ya pili, wakishinikiza Serikali kutekeleza madai yao, likiwemo la Dk Mponda na Dk Nkya kujiuzulu.
Februari 9 mwaka huu madaktari hao walirejea kazini baada ya kugoma kwa siku 17 wakishinikiza Serikali itekeleze madai yao kadhaa, likiwemo suala la nyongeza ya posho na kuwajibishwa watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Kurejea kwao kazini kulikuja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutangaza kuwasimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa.
Taarifa ya viongozi wa MAT iliyotolewa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Donbosco jijini Dar es Salaam, walisema wamemsimamisha uanachama Dk Nkya kwa kipindi cha miaka miwili na kuongeza kuwa licha ya madaktari kurejea kazini, hawako tayari kufanya kazi chini ya uongozi wa mawaziri hao.
Uamuzi kusitisha mgomo ulikuja baada ya viongozi wa Mat hicho na wale wa Jumuiya ya Madaktari kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, juzi kujadili mgogoro wao.
Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi..
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment