Home » » Kikwete awaita chemba Ikulu Madaktari...

Kikwete awaita chemba Ikulu Madaktari...



Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Mh. J. M. Kikwete jana aliahirisha kulihutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na badala yake akaitisha mkutano wa faragha na viongozi wa Chama cha Madaktari (MAT) ambao wanasimamia mgomo wa nchi nzima wakishinikiza kufukuzwa kazi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya.

Rais Kikwete alifanya kikao hicho jana mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam huku kukiwa na amri ya Mahakama ya Kazi inayowaamuru madaktari hao kurejea kazini kutokana na maombi yaliyowasilishwa na Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali, juzi.

Hata hivyo, jana madaktari hao waliendelea na mgomo kwa maelezo kuwa hawana taarifa rasmi ya Mahakama hadi walipoitwa Ikulu kuzungumza na Rais Kikwete.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kukutana na madaktari hao ambao wanagoma kwa mara ya pili, ya kwanza ikiwa kuanzia Januari 23, mwaka huu hadi Februari 9 na huu wa pili ulianza rasmi Jumatano iliyopita.

Hata hivyo, baada ya kikao hicho, hakuna upande wowote uliokuwa tayari kuzungumzia kilichojadiliwa.
Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alikataa katakata kuzungumzia kilichojiri kwenye mkutano huo na Rais Kikwete na badala yake akasema atatoa taarifa kamili na kuwweka kila kitu hadharani hivi punde.





Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger