Home » » MACHINE YA MATITI MARUFUKU TANZANIA

MACHINE YA MATITI MARUFUKU TANZANIA

Wiki chache zilizopita Wachina a.k.a wazee wa FAKE waliingiza Machine ya kufirm(kusimamisha) maziwa (manyonyo ya wamama) nchini Tanzania jambo ambalo lilikimbiliwa na wakazi mbalimbali jijini Dar es Salaam mitaa ya Sinza kwenye salun moja mitaa hio...

Baada ya habari hizi kufikia ngazi za juu nchini waziri wa afya amesikika akiipiga marufuku machine hio nakudai kwamba inaashiria hatari hapo mbeleni na ametuma wataalam wakaguzi waende kukagua chombo hicho na kutoa majibu kama hakina noma na madhara kwa binadamu ndio kitaruusiwa ; Aidha wamiliki wa vyombo hivyo wamepigwa stop mpk uchunguzi utakapokamilika..

Wamama wengi wamesikika wakisema kua chombo hiko kimekaa kihatarihatari kwani kinachomekwa kwenye umeme alafu hivyo vibakuli vinachomekwa katika matiti na unatakiwa ukae hapo kwa muda wa dk 45 na kwamba ni karibu sana na moyo ..kwahio lazima kutakua na side effect za kiafya hapo mbeleni....

Mchina mtaalamu wa chombo hicho amesema kua hata baada ya maziwa kusimamishwa na machine hiyo kuna kipindi yatakuja kuachia ngazi tena kwahio mtumiaji anatakiwa kurudi tena kwa Mchina mara kwa mara jambo ambalo limezidisha mixed feelings kwa baadhi ya watumizi wa machine hio.....

Mweeh chonde kina mama fanyeni uchunguzi au subirieni uchunguzi kabla hamjakimbilia kupata saa sita kasorobo alafu baadae zikaja kuwa saa kumi na mbili na dk 45 na hamu yenyewe ya urembo ukawatokea puani....mweeh


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger