Home » » AJIRUSHA TOKA GHOROFA YA 14

AJIRUSHA TOKA GHOROFA YA 14

Pichani wajeda wakiubeba mwili wa mwanamke aliyejirusha toka ghorofani:

Mwanamke mmoja alietambulika kwa jina la Justine Nalugya mwenye umri wa miaka 26, alifikia umauti wake jana mchana alipoamua kujirusha kutoka kwenye ghorofa ya 14 katika jengo la Workers House la NSSF nchini Uganda..

Mdada huyo inasemekana alionekana mchana huo aki-sign in hapo reception na kujieleza kua alikua anaenda kuonana na jamaa mmoja aitwaye Peter na kupewa ki-visitor pass chake na kuishia kwenye lift. Baadhi ya wafanya kazi wa jengo hilo  wanadai kwamba baada ya muda walimuona dada huyu akiwa amesimama kwenye Balcony na akiwa katika style ya kujiandaa kuruka ila walidhani anatania..

Mfagiaji wa jengo hilo pia alishuhudia kumuona m-dada huyo akirusha mkoba wake chini, kutoka hapo ghorofani akifuatia na kurusha viatu vyake then akapandisha sketi yake kwa juu na ku-dive angani utasema alikua naekti muvi......walipokuja ground floor kuchek shuhuda mmoja anasema yule dada alipotua chini hakusogea wala kusema  neno moja alikua kashafariki dunia....na kichwa kilifumuka na ubongo wote out....

Mpaka leo hii bado police inaendelea na uchunguzi maana hakuna aliepata bahati ya kujua yaliyomsibu bi dada mpaka kuchukua uamuzi wa kuondoa uhai wake, aidha wakazi wa Kampala wamesikika wakihoji kulikoni? hilo jengo lina matatizo gani kwani hii sio mara ya kwanza mtu kujiua kwa kuruka katika same building na katika same floor, aidha watu wameanza kutilia mashaka jengo hilo na kutaka police wafanye uchunguzi haraka wa kubaini kunani katika mjengo huo.....
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger