Hatimaye wachunguzi wamepata kupumzika baada ya kugundua chanzo halisi cha kifo cha mwanamama Whitney Houston, Ingawa ilishasemekana kua alikutwa amezama kwenye bafu la kuogea, kuna baadhi ya wadau waliodai kua pengine alifanyiwa kamchezo na hivyo kupelekea watu wengi watake uchunguzi wa kina kuthibitisha kua hakukuwa na mkono wa mtu kuhusiana na kifo cha mwanamuziki huyo mashuhuri
Report imeonyesha kuwa kweli Whitney alikufa kwa kuzama kwenye bath tab baada ya kuwa-high kwani wataalamu wamekuta madawa mbalimbali katika system ya Whitney dawa hizo ni pamoja na Xanax, ambayo ukinywa inakufanya uwe high kiana, na pia walikuta bangi ambapo iliwashangaza kwani alidai ameacha vyote hivyo..
Kwa taarifa hio familia ya marehemu imebidi iridhike na uchunguzi na kuendelea kumuombea mpendwa wao a-rest in peace. Blog ya sweethome bado ipo katika masikitiko makubwa ya kumpoteza mwana intataimenti huyu na pia inamtakia ku-R.I P Miss Houston..
0 comments:
Post a Comment