Haya tena wenye pesa zao wameonea huruma Jeshi letu la Police Tanzania kwa kutokua na vifaa vya kuwasaidia kazi zao za kipolice za uchunguzi mbalimbali nchini na hivyo kuwamua kuwasponsa na maikwipument ya ukweli ili kusaidia usalama wa Taifa nchini bongoland a.k.a Tanzagiza...
Maikwipument yenyewe ni pamoja na malamputompu (laptop) na ma digital camera, printer na majenereta ya ukweli kabisa ili kusaidi Jeshi letu lenye vifaa duni vya utendeaje kazi......Makabidhiano hayo yalioambatana na kijiparty cha hapa na pale huko Ubalozi wa U S and A nchini Tanzania...
Kwa niaba ya Watanzania blog hii inatoa shukrani kwa Wamarekani hao na waendelee na moyo huo huo wa utoaji kwani ni kweli tunahitaji msaada...
0 comments:
Post a Comment