Home » » MTOTO MCHANGA MWINGINE ATUPWA HUKO IRINGA...

MTOTO MCHANGA MWINGINE ATUPWA HUKO IRINGA...



Wananchi  wakiwa  wameubeba mwili  wa mtoto huyo baada ya  kutupwa 
MTOTO anayekadiriwa kuwa wa umri wa miezi sita amekutwa amefariki dunia baada ya kutupwa na mtu asiyefahamika. Tukuio hilo limetokea leo majira ya saa 7:30 mchana katika eneo la shule ya msingi ya Mtwivila manispaa ya Iringa.
 
Mashuhuda watukio hilo wamesema kuwa tukio hilo ni lapili kutokea katika kata hiyo wakati tukio lingine lilitokea wiki mbili zilizopita “haya matukio tumechoka nayo wanawake wamekuwa wauwaji hawana hata hofu ya Mungu tukio hili jamani sio lakwanza wiki mbili zilizopita tumeokota mtoto katika kata hii kwanini wanashika mimba kama hawajajipanga”alisema Rukia Juma.

 
Naye Edina Coster alisema kuwa kitendo chakutupa watoto kinasikitisha ndani ya mkoa wa Iringa kwakuwa sasa imekuwa kama mchezo”kama hivi leo ametupwa mtoto huyu wakiume ambae huenda angekuwa kiongozi  hapo mbeleni inauma sana” alisema.  Kwa upande wake Zakaria Mufuga alisema kuwa ugumu wa maisha na kutojipanga katika uzazi imekuwa ni sababu kubwa ya watoto kutupwa” hili tatizo la kuendekeza ugumu wa maisha ndio sababu ya watu kugeuka wauwaji unakuta mtu anapenda starehe lakini kupanga uzazi hawezi matokeo yake anashika mimba isiyo tarajiwa anatupa mtoto huu ni ukatili mkubwa”alisema

“Watu wanatafuta watoto kwa hospitali na kwa waganga wa jadi hawapati dada zetu mnapata mimba mnatoa hivi kwanini msifunge tu vizazi muwe huru” alisema Emmanuel Msungu. Mmoja wa wazazi Charles Sia aliyebeba kiumbe kwenda kukistiri alisema kuwa wazazi wanachangia tatizo la utupwaji kwa watoto kutokana nakutokuwa na upendo na familia zao”wazazi tupunguze ukatili kwa watoto wazazi tumekuwa wakali kiasi ambacho mtoto anapata ujauzito anaogopa kusema na matokeo yake wanatoa mimba nakuwatupa watoto kama takataka. 

 
Mzazi mwingine aliyeshindwa kuzuia machozi yake alisema kuwa wazazi wanapata tabu kuwalea halafu wao wanageuka kuwa makatili na kuwatupa watoto”wanaotupa watoto hatuwataki sisi tunapata tabusana kuwalea kwanini mnatupa watoto. Mzee huyo alimalizia kwa kwi kwi ya kulia na kusema kuwa Mungu amuweke mahala pema mtoto huyo kwa kuwa ni malaika ambaye hajamkoesa mtu. 


Habari kutoka Lindiyetu.blogspot na Na Zuhura Zukheli
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger