Askari wa pikipiki maarufu kama 'Voda Fasta' walifika eneo la tukio na kumuokoa kibaka huyo asiendelee kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira…
Kibaka aliyetaka kumpora denti wa kidato cha sita shilingi milioni tatu akiwa hoi baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi eneo la Area Five jirani na kituo cha Oil Com kilichopo maeneo ya Nane Nane mkoani Morogoro leo.
Mwanafunzi huyu ndio alienusurika kuibiwa pesa zake kiasi cha sh mil 3 za ada alizotumiwa na wazazi wake huko Morogoro . Denti huyo alifanikiwa kumkabilia kibaka huyo mzoefu na kupiga makelele ya mwizi ndio wananchi wenye hasira kali wakamkamata na kumfanyizia kibaka huyo ambaye aliokolewa na police mikononi mwa wadau wenye machungu na vibaka kama hawa....
PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE -MOROGORO - GPL
0 comments:
Post a Comment