Home » » UTUMIKISHWAJI WA WATOTO KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI BADO TATIZO KANDA YA ZIWA

UTUMIKISHWAJI WA WATOTO KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI BADO TATIZO KANDA YA ZIWA

HAPA NIKIZUNGUMZA NA MTOTO MWENYE MIAKA NANE AMBAYE ANAFANYA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI WA DHAHABU KATIKA MACHIMBO HAYO.
 
GEITA
Tatizo la utumikishwaji wa watoto katika baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa yanayojishugulisha na uchimbaji mdogo wa madini limeendelea kuwa sugu kufuatia jamii kutokuwa na elimu juu ya athali za ajira hatalishi kwa watoto.

Hayo yamebainishwa leo na baadhi ya wachimbaji na wanunuzi wa dhahabu walipokuwa wakiongea na Blog hii katika machimbo madogo ya shenda yaliyopo wilayani Bukombe mkoani Geita.

Wamesema kuwa katika machimbo ya Shenda kuna watoto zaidi ya ishirini wanaofanya kazi ngumu kwa ujira mdogo huku wakikumbana na matatizo mbalimbali yakiwemo magonjwa na njaa.

Mmoja wa wanunuzi wa dhahabu katika machimbo hayo Bwana Amocy Mapiga amesema kuwa mara kwa mara viongozi wa wamekuwa wakitembelea eneo hilo na wala hakuna kiongozi aliyetilia mkazo na kutoa elimu kwa jamii kuhusu athali hizo.

Kwa upande wao baadhi ya watoto waliongea na blog hii wamesema kuwa wazazi wao ndiyo wanaowatuma ili waweze kupata pesa kwa ajili ya kununulia mahitaji muhimu ya nyumbani.

Katika hatua nyingine wachimbaji hao wamesema kuwa swala la ngono zembe limekuwa ni jambo la kawaida katika eneo hilo kutokana na ugumu wa mazingira  hivyo kuiomba serikali kufika kutoa elimu mara kwa mara ili kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi.

MATUKIO KATIKA PICHA

HAPA NIKIWASILI KATIKA ENEO LA MACHIMBO MADOGO YA DHAHABU KATIKA KIJIJI CHA SHENDA WILAYA YA BUKOMBE MKOANI GEITA
MAENEO YA ARDHI YA KIJIJI CHA SHENDA YALIVYOHARIBIKA KUTOKANA NA UCHIMBAJI WA DHAHABU.

MAMA MWENYE UMRI WA MIAKA HAMSINI AKIWA AMELALA BAADA YA KUCHOKA KUPASUA MWAMBA.

MTU NA MKE WAKE KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA DHAHABU.

ONA JINSI MTI HUU ULIVYO KATIKA HATARI YA KUFA BAADA YA UDONGO WOTE WA MIZIZI KUCHIMBWA.

MTOTO WA MIAKA NANE AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUSOMBA MAWE MAZITO KUTOKA UMBALI WA KM 1 ILI KUPATA PESA.

HUU NI UDONGO WA MASALIA BAADA YA KUCHIMBWA AMBAO UNASEMEKANA KUNA MUWEKEZAJI ANAUNUNUA NA KWENDA KUUFANYIA KAZI ZA KUTAFUTA TENA DHAHABU KWA MITAMBO MAALUMU.

HII NI SEHEMU YA KUOSHEA UDONGO ULIOCHIMBWA,NI KISIMA CHENYE UREFU WA MITA TANO,JE MTOTO MDOGO AKITELEZA HAPO INAKUWAJE?

MITAMBO YA KUSAGA MAWE ILI KUPATA UNGA WA MAWE AMBAO UTACHEKECHWA KUPATA DHAHABU.

HAPA NIKIWA MBELE YA MITAMBO HIYO NA JIWE AMBALO NIMESHIKA LITASAGWA NA MTAMBO HUO ULIOPO MBELE YANGU HADI KUWA UNGA.

KIJANA AKIWA KATIKA HATUA ZA MWISHO MWISHO ILI KUIFIKIA DHAHABU,HAPA AKICHUJA UDONGO WENYE DHAHABU KA KUTUMIA MEXURY ILI KUZIPATA.

JAMAA HAWA WAO NI WASANII WA BONGO FLAVOUR HAPA WANAKULA TIZI LA MICHANO BAADA YA KUCHOKA KUCHIMBA DHAHABU.

MAUZOOOO TU JUU MCHANGA AMBAO UMECHIMBWA ILI KUPATA MALI.

HAPA NIKIWA NA JAMAA WAKINIELEZEA HATUA YA TATU KUTOKA MWISHO JINSI YA KUITAMBUA DHAHABU KWA KUTUMIA MAGUNIA.

MNUNUZI WA DHAHABU KATIKA MACHIMBO HAYO AKIKAGUA MALI

HAPA STORY ZILIBAMBA MBAYA,HUWEZI AMNI JAMAA MARA YAKE YA MWISHO KUONA CONDOM ANASEMA NI 2009,TANGU MUDA WOTE ALIOKAA HUKO HAIJUI KABISA,Duuuuuu!!! ILA KILA SIKU LAZIMA APATE WA KUMPUNGUZIA BARIDI,

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger