Home » » MREMBO ATAKAYE IWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2012 HUYU HAPA...

MREMBO ATAKAYE IWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2012 HUYU HAPA...

                          

Mrembo atakaewakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa JOCELYNE DIANA MARO (22) katika pozi.
MREMBO huyo alipatikana kufuatia mchakato ulioendeshwa na kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa 2012
Jocelyne amehitimu shahada ya Business Economics mwezi wa saba mwaka huu katika chuo kikuu cha Keele University, Nchini Uingereza
Maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza kuvuta hisia za watu wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo wanaowania taji hilo.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.


Habari na GPL....

Yaani nimeiona hii pic i just had to put her here, she is beautiful kwa kweli, sasa sijui ni picha ama vipi, but i think she really is beautiful.....go gurl
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

2 comments:

Anonymous said...

She is beautiful. Let's hope that can be represnted
In her brains as well. Kwa sasa Africa's focus with peageants
Is "beauty with a positve purpose to society"...
Otherwise social reflections of former beauty queens kama
Jokate, wema seputa etc... Beauty peagents & queens have lost society
Respect.

Anonymous said...

Yaani ni mrembo kwa kweli Mungu amtangulie

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger