Home » » MKUNGA WA JADI AWASAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO KUJIFUNGUA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

MKUNGA WA JADI AWASAIDIA WANAWAKE WAJAWAZITO KUJIFUNGUA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU


 Mid wife a.k.a Mkunga wa Jadi Bi Agripina Namwichi(37)(kulia) akimkabidhi mtoto wa kiume Bi Shija Bundala(26) mkazi wa Kijiji cha Mbuyuni, Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume nyumbani kwa mkunga huyo. Awali mwanamke huyo amewahi kujifungua watoto kwa awamu mbili kupitia Oparesheni katika Kituo cha Afya cha Mbuyuni lakini kwa mkunga huyo inadaiwa alijifungua salama salimini licha ya kuwa na uhaba wa vifaa na eneo maalufu la kitaalamu.

Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.

Chumba maalumu kwa ajili ya kuzalia(labor)

Mkunga akiandaa eneo la akina mama wajawazito kwa ajili ya mapumziko kabla ya kujifungua.

kwa habari zaidi ingia humu: http://chimbukoletu.blogspot.com

Dah!! kiukweli hii habari imenisikitisha sana, yaani hayo mazingira ya kujifungulia yanatia huruma jamani, na MOJA YA NDOTO ZANGU HAPO BAADAYE NI KUWA NA ZAHANATI YA KUSAIDIA WATU KAMA HAWA, but again mimi kama mwananchi mmoja nitaweza kweli?!!  kwahio hii kwangu inabaki tu kua ndoto....huyo mkunga mwenyewe anaonekana kajichokea maskini, na sijui anawachaji au ndio kaamua kuwasaidia tu bure jamani, ...nchi ina uhuru miaka 50 ila bado watu tupo katika mazingira haya mweeh??? this is truly sad......nikianza kulalama hapa nitamaliza keshokutwa naomba tu niseme kwa upole kwa mara nyingine tena SERIKALI KAMA MNAWEZA(TUNAJUA SANA MNAWEZA ILA HAMJAPENDA TU KULIANGALIA SUALA HILI) Kama mkipenda CHONDECHONDE heeeeeeeellllllpppuni hawa watu mweeeeh

Ni mimi mwenye majonzi
Binti Ndonde...

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

3 comments:

Anonymous said...

Wooooo Mungu ambariki sana

Anonymous said...

Mama Mandy uko juu ma news ya kumwaga hongera

Anonymous said...

Tina fungua zahanati tutakuchangia, maana mama vijacho kweli tunapata shida sana jamani...hata kwenye mahospitali makubwa ya serikali bado uozo mtupu...

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger