Home » » REDD’S MISS TEMEKE KUZOA MIL 1.5 KESHO

REDD’S MISS TEMEKE KUZOA MIL 1.5 KESHO


Warembo wanaowania shindano la Redd's Miss Temeke 2012.

Mrembo  atakayetwaa taji la Redd’s Miss Temeke 2012 katika shindano linalofanyika Ijumaa Sept 21 katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall), atajinyakulia zawadi zinazofikia milioni 1.5 sanjari na tiketi ya moja kwa moja kushiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Katika mlolongo huo wa zawadi, mshindi wa kwanza atajinyakulia fedha taslim Sh. Milioni 1. Mshindi wa pili atajinyakulia fedha taslim Sh.laki nane wakati mshindi wa tatu atapata Sh. Laki saba na washindi wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja Sh. Laki  5.
Duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na kiatu cha Sh 150,000 kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza watakaoshinda. Mbali ya washindi hao, mshindi wa nne atajinyakulia kitita cha Sh. 400,000 ambapomshindi wa tano  ataondoka na Sh 300,000 wakati warembo wengine wote watakaosalia kila mmoja atapata Sh.200.000.
Ikiwa ni funga dimba ya mashindano ya urembo ya kanda nchini, shindano hilo litanogeshwa na wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambaye mbali ya kuigiza sauti za watu mbalimbali, pia ametoa filamu kadhaa kwa siku za hivi karibuni.
Shoo ya ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine yeyote iliyowahi kuyanyika nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini msichana anatakiwa kufanya na si unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Picha na habari toka GPL
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger