Home » » MWANDISHI WA BLOG YA FRANCIS GODWIN AAMUA KUJIFICHA KWA KUHOFIA MAISHA YAKE KWANI ALISHUHUDIA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI LIVE BILA CHENGA.....NA AMESEMA ATATOA USHAHIDI WOTE

MWANDISHI WA BLOG YA FRANCIS GODWIN AAMUA KUJIFICHA KWA KUHOFIA MAISHA YAKE KWANI ALISHUHUDIA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI LIVE BILA CHENGA.....NA AMESEMA ATATOA USHAHIDI WOTE

                           
Francis Godwin na my wife wake wakiwa kwenye basi wakielekea chimbo kwa muda usiojulikana

Habari hii nawaletea kama nilivyosoma na kukopi na kupesti taarifa hii kutoka kwenye blog yake; kwamba Francis ni mmoja moingoni mwa mashuhuda walioshuhudia ukatili wa mapolice waliomuua Mwandishi mwenzie majuzi huko Iranga, amekua akiwindwa na wajeda hao ili kutolewa uhai wake kwa kua ana siri nzito ya tulio hilo full  HD kwani alikua mwanzo mpk mwisho wa tukio, namnukuu kama ifuatavyo; 

 '' Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa''. Mwisho wa kunukuu.


Haya tushajua mnachotaka kukifanya nyie wahusika sasa ole wenu mumrestishe in pisi na huyu muone mziki wake, maana mtakua mmezidi na wananchi safari hii hawatakubali.......sijui kama Serikali mnafuatilia hii habari sijui

Sosi: http://www.francisgodwin.blogspot.com/


Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi na mkewe ni huyo mwenye vitenge na t-shirt nyeupe ambaye pia ni dada yake marehemu Daudi Mwangosi,


Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na  kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli  wanamtafuta Godwin na wenzake.           
Namkariri Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”

 Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari wengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger