Home »
» ANAYEDAIWA KUMLIPUA MWANGOSI ASHIKILIWA NA POLICE
ANAYEDAIWA KUMLIPUA MWANGOSI ASHIKILIWA NA POLICE
YEYE, WENZAKE WANNE WANASHIKILIWA POLISI IRINGA, KITANDANI NI ASKARI ALIEUMIA MGUU BAADA YA BOMU WALILOMLIPULIA DAUDI KUMJERUHI NA YEYE.
ASKARI watano wa Jeshi la Polisi akiwamo anayetuhumiwa kumlipua kwa bomu Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo mkoani Iringa. Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao imekuja siku moja baada ya kubainika kwamba, askari kadhaa walioendesha operesheni dhidi ya wafuasi wa Chadema mkoani Iringa na kusababisha kifo cha Mwangosi walitoka mikoa ya Dodoma, Mbeya na Morogoro.
Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya askari polisi mkoani Iringa na Makao makuu jijini Dares Salaam, zilisema kuwa polisi hao, akiwamo yule aliyeonekana kwenye picha za video na za mnato akimlipua kwa mtarimbo wa bomu la machozi (jina tunalo) wamekamatwa na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Iringa.
Kwa mujibu wa habari hizo, askari hao walikamatwa Jumatatu wiki hii ikiwa ni siku moja baada ya mauaji hayo yanayoaminika kufanywa na Jeshi la Polisi kwa kutumia askari wa mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani. "Hivi sasa (jana mnamo saa 8:30 mchana) ninapozungumza na wewe bado hao askari wanaendelea kuhojiwa. Wako watano," alisema askari polisi mmoja aliyekuwa karibu na chumba wanachoshikiliwa askari hao.
Chanzo hicho kilieleza kuwa askari aliyemuua Mwangosi alionyesha kusikitikia tukio hilo akisema hakukusudia kufanya hivyo.
"Anasema ni kwamba, yeye mwenyewe hakupenda kuona tukio hilo likitokea. Aliniambia kuwa kifo cha mwandishi huyo kimemsikitisha sana, na nilipomuuliza nini hasa kilitokea, alisema; ahh hilo niache nitaeleza nitakapohojiwa," kiliongeza chanzo kilichokuwa karibu na askari huyo.
Afisa Upelelezi wa Ukoa wa Iringa, (RCO), SSP Nyigesa Wankyo hakuthibitisha kuwashikilia askari hao, badala yake akataka kazi hiyo ifanywe na polisi Makao Makuu. Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo na simu yake ya mkononi haikuwa inapatikana hadi tunaenda mitamboni.
Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kamishna Robert Manumba alisema; "Wakati ukifika mtaambiwa. Kwa sasa muda haujafika, subirini uchunguzi uendelee, mtaambiwa".
Polisi aliyelipuliwa mguu anena
Katika hatua nyingine, mmoja kati ya askari waliokuwapo wakati tukio zima lililosababisha kifo cha Mwangosi ambaye alijeruhiwa katika mguu wake wa kushoto na kupoteza fahamu kabla hajafikishwa hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa anaendelea vizuri na matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo, Aseri Mwampamba alisema alipoteza fahamu baada ya kujeruhiwa katika mguu wake wa kushoto.
"Ni kweli nilikuwa eneo la tukio baada ya kuona hali ya amani katika eneo hilo imekuwa si nzuri, wanachama hawakutaka kuondoka eneo la mkutano. Wakaanza kufanya vurugu na kusababisha nikajeruhiwa mguuni kama unavyoona," alisema Mwambapa.
Alipotakiwa kueleza majeraha hayo aliyapataje, askari huyo alisema hata yeye hafahamu isipokuwa akiwa amesimama alishangaa kuona kitu kikitua mguuni na kwamba anadhani kilitoka chini na kutua katika mguu wake wa kushoto.
Hata hivyo, picha za mnato zilizochapishwa kwenye magazeti mbalimbali nchini baada ya tukio hilo, zimeonyesha kuwa mara ya mwisho Mwampamba alionekana amekumbatiwa na marehemu Mwangosi huku askari mmoja alilenga mtarimbo wa kufyatua mabomu ya machozi.
Habari zaidi ingia Mwananchi...
Haya sasa mmeshawakamata mtudanganye sasa wametoroka maana tunajua ni watu wenu wala hamtawafanya kitu....mmmxxxxxhhh Dhaifu pyuuuuuuuu
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment