Home » » USAFIRI WA TRENI TANZANIA

USAFIRI WA TRENI TANZANIA

BAADA ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.Unakuta nauli halali ni Sh9,000 lakini, abiria ameandikiwa Sh29,000.Pia ameagiza kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka3 hadi 10 na pia kuondolewa kwa malipo ya mizigo midogo ya abiria. (Picha na maelezo kutoka kwa mdau mmoja huko fb)


Sasa hapa sijaelewa kwanini mtu anapanda treni kwa kudandia hivi kama dala dala jamani? unajia sasa ndio napata picha kuna siku rafiki yangu mmoja Mrwanda alinitania na kusema ''aah Treni za Tanzania bwana kwenye vituo hakuna maplatiform na tren inasimama mahali popote watu wanakimbilia kuingia hadi madirishani''.

 Nilim-bishia sana maana ki ukweli sijawahi kutumia usafiri wa tren TZ so sikujua mazingira yake. Ila sasa ninapoona picha na kusikia maelezo ya watu kwanini TRL hawatengenezi vituo vya tren jamani nasikia watu wengi sana wanatumia huu usafiri, kwanini bado watu wanapanda tren kwa style kama hii??  Jamani mi nimeshachoka na hii Serikali kila siku narudia kuuliza maswali haya haya hakuna anaejibuuuuu mweeeeehhhhh
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger