KUFUATIA taarifa kuwa, dawa za Kichina za kuongeza makalio zina madhara kwa watumiaji, njia mbadala ya kukuza maeneo hayo nyeti imegunduliwa na imeanza kutumika kwa kasi Bongo, Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu (wa gazeti la Amani) umebaini kuwa njia hiyo inayotumiwa kwa sasa na wanawake wengi hasa wa mjini si ya kumeza wala kupaka dawa bali ni ya kuvaa taiti zilizojaladiwa vifaa maalum vilivyotuna mithili ya makalio.
Jinsi inavyokuwa
Akizungumza na Amani, mmoja wa wafanyabiashara wa ‘makalio’ hayo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sanura, alisema ubunifu huo umekuja kufuatia utafiti kuonesha kuwa baadhi ya wanawake wanatamani kuwa na makalio makubwa ila wanaogopa kutumia dawa za Kichina.
''Wanawake wengi wanatamani kuwa na makalio makubwa ili wawadatishe wanaume lakini hawakujaaliwa kuwa nayo, wapo ambao wamefikia hatua ya kutumia zile dawa za Kichina na ilipobainika zina madhara wameacha. “Watu wakakaa na kuumiza vichwa, na walipogundua njia hii ambayo ni salama kwani anachotakiwa kufanya mwanamke ni kununua taiti hizo ambazo ndani yake kuna kina kitu chenye shepu ya kalio na hips, akivaa na suruali au sketi, huonekana amejaaliwa kumbe hamna kitu,” alisema mama huyo mwenye duka lake la nguo maeneo ya Kariakoo, Dar.
Habari zaidi ingia Global Publishers
Hivi mbona wanawake wanahangaika sana kuwadatisha wanaume, je na wanaume nao wanahangaika hivi kudatisha wanawake? mweeh........am just thinking out aloud......
0 comments:
Post a Comment