Home » » SAMAHANI KWA PICHA : POLISI MSTAAFU AMCHARANGA MWANAE WA MIAKA 4 KWA MAPANGA

SAMAHANI KWA PICHA : POLISI MSTAAFU AMCHARANGA MWANAE WA MIAKA 4 KWA MAPANGA


polisi-amcharanga-mapanga-mwanae-miaka-4-picha-2

HUZUNI: MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA

Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness Elius (28) huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.

Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.

Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.

Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.

Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.

Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.


                    
               Mtoto Devotha akihudumiwa na wauguzi kujaribu kumuokoa maisha yake

                   Uuuwwii pole mtot mzuri Mungu atakuponya jamani.....( am sobbing for the pain this lil angel is going thru)
polisi-amcharanga-mapanga-mwanae-miaka-4-picha-0

                    Mtuhumiwa akiwa hoi hospitalini baada ya kupokea kichapo kutoka kwa majirani wenye hasira
ASKARI POLISI MSTAAFU SAMSON BWIRE AKIWA AMEFIKISHWA HOSPITALINI MDA MCHACHE BAADA YA KURUKA KUTOKA KWENYE GARI AKIJARIBU KUKIMBIA. Ambapo alipatiwa kisago cha ukweli na majirani wenye hasira kali...
                            

 Mtuhumiwa akiwa hoi hospitalini baada ya kupokea kichapo kutoka kwa majirani wenye hasira (wangelinyofoa na maini kabisa, baba gani unaweza kumfanya mwanao hivi kweli? )                           
   KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.

NEWS UPDATE:  MTOTO DEVOTHA GERALD AFARIKI DUNIA


HABARI NILIZOZIPATA SASA HIVI BAADA YA KUPOST HIZI HABARI NI KWAMBA MTOTO DEVOTHA HUYU ALIEUMIZWA HIVI NA BABA YAKE HATIMAYE AMEFARIKI DUNIA MASKINI YAANI ROHO INANIUMA JAMANI UUUWWIII JAMANI UUWWWII NALIA KWELI MASKINI OOOH GOD MTOTO WA WATU MPUMZISHE KWA AMANI JAMANI....OOH NO I HAVE TO STOP I CANT WRITE ANYMORE..... DAAH INAUMA MNOOO...


R.I.P BABY DEVOTHA




Habari na picha hizi kwa hisani ya http://bundalawilliam.blogspot.com
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger