WABUNGE katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walihudhuria mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), walipata msoto wa nguvu.Tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kwamba wabunge hao wangepewa mafunzo kwa kubembelezwa kutokana na nafasi zao, walikutana na msoto wa nguvu mwanzo hadi mwisho.
Kuonesha jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu, katika kambi ya Tanga, siku tu ya utambulisho, mbunge wa Chadema (jina tunalo), alizimia.
MAFUNZO YANA FAIDA?
Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi kikubwa. “Japo ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi, program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.” Kwa upande wa Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe anapitia mafunzo ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia yanakupa uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”
Credit: GPL
0 comments:
Post a Comment