Pichani ni wajawazito wakiyoka kwenye semina
WAHUDUMU 886 katika wilaya ya Bariadi na Itilima wamekabidhiwa simu na shirika la Tiba na Utafiti (AMREF) kwa ajili ya kurahisisha ukusanyaji wa taarifa za mama mjamzito katika jamii.
Akizungumza na Habarimpya.com baada ya semina ya matumizi ya simu hizo kuhusu namna ya kumuandikisha mama mjamzito na kukusanya taarifa zake kupitia simu Meneja wa mradi huyo wa Uzazi na Uzima Dk Benatus Sambili alisema simu hizo zitawasaidia kupata taarifa sahihi kuhusu takwimu za wajazito katika maeneo yao.
“Tunawaelekeza hawa wahudumu jinsi ya kukusanya takwimu za mama mjamzito kupitia simu ambapo mama atakuwa anakumbushwa kwenda clinic na kufahamu Afya ya Uzazi na nini anatakiwa kukifanya ili kunusuru vifo hivi” alisema Sambili.
Aidha Sambili alisema kuwa mradi huo umefadhiliwa na Shirika la misaada (Cida) ndani ya miaka mitatu na nusu ambapo awali walianza kuwagawia baiskeli 1000 na vifaa mbalimbali wakiwa wahudumu 1995 katika mkoa mzima na sasa wameamua kuwasaidia simu kuhakikisha vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga vinapungua mkoani humo.
Sambili alisema kuwa jumla ya simu ni 886 aina ya samusang zenye thamani ya sh.35millioni zinazotumia mtandao wa Airtel ambapo alisema kuwa japo mtandao ulikuwa shida katika kufanikisha Elimu hiyo lakini sasa wahudumu hao wanaelewa juu ya utumiaji wa elimu hiyo.
Habari na Annastazia Fredy,Bariadi -Simiyu kutoka Habarimpya.com
daah safi sana aisee mdogo mdogo kama hivi tutafika tu, am so happy for hawa wamama yaani , na-wish tungeweza kufanya hivi Tanzania nzima yaani ila ndio tushaanza hivyo..safi kabisa.....asanteni sana wadhamini wa program hii.
0 comments:
Post a Comment