Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Imebainika kuwa Wanawake wengi
kushindwa kusimama na kutetea haki zao kumetokana na kutojua Sheria za ndoa,
Mirathi na uandikaji wa Wosia baada ya kufiwa na Waume zao.
Hayo yalibainishwa jana na
Mratibu wa Kitengo cha Msaada wa Sheria
kwa Wanawake na Watoto (MBEPAU) Jane Lawa wakati wa Semina iliyotolewa na
Shirika hilo kwa Vijana, Wajane, Wagane, Viongozi wa Kimila na Dini
iliyofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden Mkoani hapa kwa ufadhili wa Asasi
ya The Faundation for Civil Society.
Lawa
alisema lengo la Semina hiyo ni kuiwezesha jamii kujua sheria ya ndoa, mirathi
na uandikaji wa wosia baada ya kugundulika kuwa watu wengi wanashindwa kusimama
mahakamani na kutetea haki zao kama talaka na mirathi hususani wanawake.
Aidha
alisema Semina hiyo ni ya mwisho kufanyika kutokana na ufadhili wa Asasi ya The
Faundation baada ya kufanya kwa awamu nne kwa kata zote za Jiji la Mbeya ambapo
alizitaja kata zilizomalizia kuwa ni pamoja na Ilemi, Iyela, Nonde, Tembela na
Mwasanga.
Alisema
MBEPAU walianza kutoa elimu katika jamii kwa lengo la kuijengea uwezo wa
kutambua haki zao baada ya kuona jamii ina uelewa mdogo wa kisheria na haki
zao.
Hatua
hiyo inakuja baada ya wanawake wengi na watoto maeneo ya vijijini kudhurumiwa
haki zao kutokana na kuto tambua haki zao za msingi zikiwemo haki ya kumiliki
Ardhi na mali,haki za watoto na elimu ya ndoa.
Lawa
alisema kutokana na kutambua uwepo wa tatizo hilo, wameshatoa mafunzo hayo kwa
washiriki ambao kati yao ni Maafisa
watendaji wa kata,wenyeviti na Makatibu wa mabaraza ya usuruhishi kwa wilaya ya
Mbeya mjini.
Alisema
tangu kuanza kwa mpango huo unaofadhiliwa na Tasisi ya The foundation for civil
Society(FCS) umeweza kutoa elimu kwa washiriki hao kutoka kata zote za Jiji la
Mbeya wakiwemo wajane,Walemavu, Wazee wa
Mila na vijana.
Lawa
alisema wanawake wengi wamekuwa wakipata manyanyaso mengi baada ya kufiwa na
waume zao kutokana na kutojua haki zao kutokana na kukandamizwa na sheria za
kimila za makabila yao.
Kwa
upande wake baadhi ya Washiriki wa semina hiyo walisema Serikali inatakiwa
kuunga mkono juhudi za asasi binafsi zinazotoa mafunzo na elimu kwa jamii
zilizosahaulika kama walemavu.
“ Mara
nyingi walemavu husaulika katika mafunzo kama haya lakini Serikali inatakiwa
iwe inatoa elimu kama hizi vijijini pia nawasihi walemavu wenzangu kutojificha
majumbani kwa sababu wanakosa mambo mengi” alisema Elizabeth Mwanjala makazi wa
kata ya Ilemi mshiriki wa semina ambaye pia ni mlemavu.
Kiongozi
wa Mila Nicholaus Sinjinga(85) aliyehudhuria
mafunzo hayo alisema mafunzo kama hayo yawe yanatolewa mara kwa mara ili
jamii iachane na mila zilizopitwa na wakati badala yake wafuate sheria
zinavyotaka.
Naye
Imelda Mbwilo(25) mkazi wa Tembela aliyewakilisha kundi la vijana alisema watu
muhimu wa kupewa mafunzo kama hayo ni vijana ambao wanatakiwa baada ya kupewa
elimu kwenda kutoa kwa wengine ili kujenga kizazi kitakachokuwa kinajua umuhimu
wa sheria hiyo.
Aliitaja
Sheria ya Mwaka 1971 kifungu cha 39 kinachosema ndoa ni maamuzi ya hiari kati
ya mume na mke kukubaliana kuishi pamoja hivyo suala la ndugu kuingilia masuala
ya mirathi hususani kwa wanawake wanaofiwa na waume zao kuwa yanapingana na
sheria
0 comments:
Post a Comment