Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
JESHI la polisi
Mkoani Mbeya limefukuza kazi Askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma
za kufanya mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha
polisi cha mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Kwa mujibu
wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Athuman Diwani askari huyo alitenda kosa hilo Novemba
21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya
naye mapenzi alikuwa anakabiliwa na kosa
la wizi.
Kamanda
Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa
katika mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha
alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvuliwa na jeshi la polisi na kwamba
atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo
alitopa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za
jeshi la polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kuinda maadili ya jeshi la
polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia
sheria.
Akizungumzia
tukio hilo baba mzazi wa askari huyo
alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambaco kimetia
fedheha familia yake lakini pia kwa jeshi la plisi ambalo limepewa dhamana ya
kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati huo huo katika kijiji cha malangali barabara ya Mbeya Iringa
Wilaya ya Mbarali gari yenye namba za usajili DFP 7322 aina ya Nissan Patrol
lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisa kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa
marehemu bado haujafamika na mwili
umehifadhiwa katika hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua
mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment