Jeshi la polisi Mkoani Mbeya limelazimika kufanya
kazi ya ziada kumuokoa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hawa Mwalongo (30),
mkazi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo, Jijini Mbeya.
Tukio hilo limetokea Mei 4 mwaka huu majira ya
Alfajiri mtuhumiwa akiwa na mwanae Alfonce Mwalongo (miezi mitano), alikutwa
akiwa uchi huku mwanae huyo akiwa mita chache kutoka kwenye nyumba aliyopanga
inayomilikiwa na Bwana Mashaka Seke.
Mmoja kati ya mashuhuda ambaye ni jirani yake
amesema walisikia mtoto akilia alfajiri ndipo waliamua kutoka nje na kumkuta Bi
Hawa akiwa mtupu na walipomsemesha, alisema anatoka Bunju Dar es salaam na
kwamba anelekea Mbeya na alipoulizwa nguo zipo wapi hakuwa tayari kueleza na
kutoelewa kinachoendelea.
Ameongeza kuwa amesafiri na lori lililokuwa na
Container na kufika hapo baada ya kufukuzwa na baba yake mlezi aitwaye Esco
Sikazwe, baada ya kutelekezwa na mumewe Bwana Nikas Mwalongo.
Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo
alitelekezwa na mumewe kutokana na ujauzito wa mwanawe Alfonce, kisha kuhamia
kwa baba yake mlezi ambaye alimfukuza kutoka Mtaa wa Mwakibete jijini hapa hali
iliyomlazimu kwenda kupanga eneo la Ilemi majuma mawili
yaliyopita.
Kwa upande wake Balozi Lukas Mwakalonge
alitoa taarifa kituo cha polisi majira ya saa moja asubuhi, eneo la tukio na
kumchukua mwanamke huyo na wanawe wawili Seif Mwalongo (2) na Alfonce na
kuondoka nao na kwenda Kituo cha Polisi Kati baada ya wananchi wenye hasira kali
kutawanywa na Polisi ambao walikuwa na nia ya kumpiga mwanamke
huyo.
Aidha, amesema kuwa alimpokea Bi Hawa baada ya kuletwa na Peter John ambaye walikuwa wanafanyakazi pamoja katika moja ya Vyuo vikuu jijini Mbeya kama mhudumu wa mazingira katika chuo hicho.
Hata hivyo Bibi Mmoja Sandubwe Nabwike
(90) ameowaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo
kutasababisha mauaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia kwani hata yeye ameshawahi
kuzushiwa kuwa ni mshirikiana na kutengwa, lakini baada ya uchunguzi akabainika
kuwa si mchawi.
Hili ni tukio la tatu kwa wanawake kuhisiwa ni
washirikina lakini baada ya kufikishwa hospitalini ilibainika kuwa ni wagonjwa
wa akili, akiwemo Mwalimu mmoja aliyewahi kusoma Chuo Kikuu cha TEKU.
Habari Kutoka http://chimbukoletu.blogspot.com na Ezekiel Kamanga, Mbeya.

0 comments:
Post a Comment