MTOTO wa siku moja mnamo Mei 24, mwaka huu ameokotwa katika makaburi ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya mfuko wa rambo.
Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zilidai kuwa, mtoto huyo alisikika akilia na wasamaria ambao siku hiyo usiku walienda na kumkuta akiwa katika mfuko mweusi huku mbwa wakimnyemelea.
Mtoto huyo wa kike baada ya kuokolewa na wasamaria wema alipelekwa kwenye kituo cha afya kiitwacho Afya Bora ambapo wafanyakazi wake, Catherine Shayo na Magreth Masanja walimpa huduma ya kwanza kisha wakatoa taarifa Kituo cha Polisi Buguruni na kupewa kumbukumbu namba BUG /RB/6238/2012.
Baadaye mtoto huyo mchanga alipelekwa katika Hospitali ya Amana na PC Nel.
Uchunguzi unaonesha kwamba, maeneo ya Buguruni na Vingunguti yanaongoza kwa utupaji watoto ambapo Aprili 27 na Mei 4, mwaka huu watoto wawili waliokotwa mmoja akiwa amefariki.
Habari na Makongoro Oging kutoka Global Publishers
0 comments:
Post a Comment