Home » » BIG BROTHER AFRICA KUANZA KESHO SAFARI YA 90DAYS

BIG BROTHER AFRICA KUANZA KESHO SAFARI YA 90DAYS

MSIMU mpya wa shindano la Big Brother umeanza kutimua vumbi na shindano hilo litang'oa nanga rasmi kesho, baada ya lile la mwaka jana lililomalizika Julai Mosi na Karen na Wendal kuondoka na mamilioni ya pesa.

Mkurugenzi wa M-Net, Biola Alabi amesema kama ilivyo kawaida ya shindano hilo ambalo huboreshwa kila mwaka, safari hii limeongezwa ubora mara dufu. Amesema kuwa timu imejiandaa kuwaburudisha waafrika ambao ndio walengwa wakuu wa shindano hilo ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka tano mfululizo.

Shindano hili linafanyika kwa mara ya saba mwaka huu na Tanzania ikiwa mshiriki kwa miaka sita mfululizo. Ndilo shindano pekee barani Afrika linaloonekana 'Live' saa 24 ndani ya miezi mitatu na kutazamwa na watu katika nchi 47.
Wanzania waliowahi kushiriki katika shindano hilo ni  Mwisho Mwampamba, Richard, Latoya, Elizabeth,Bhoke na Lotus.

Zawadi
Zawadi inayoshindaniwa mwaka huu ni dola za Marekani laki tatu ambayo ni wastani wa shilingi za Tanzania milioni 480. Ingawa safari hii wanaingia washiriki wawili wawili lakini tunaambiwa ni mshiriki mmoja tu ndiye atakayeibuka mshindi.

'Host' wa Kipindi
Kwa mara nyingine, IK Osakioduwa ataongoza shoo zote za 'season' hii. Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Ik kuiongoza shoo tangu alipoingia mwaka 2009.


Jumba la BBA
Safari hii jumba limenakshiwa kivingine kabisa, Biggie anasema kila kitu kimewekwa kwa maana yake, hakuna kitu kinachoonekana ndani ya jumba hilo bila kuwa na sababu, ni ndani ya siku tisini itajulikana maana ya fenicha na mapambo yaliyopo humo ndani.

Katika kila kona ya jumba hilo kuna kamera ambazo kwa ujumla wake ziko 53 na vipaza sauti 120 ili kuweza kutoa usikivu mzuri hata pale washiriki wanapoamua kunong'onezana.

J ColeNdiye msanii anayetarajiwa kusababishwa wakati wa ufunguzi wa shoo hiyo hapo kesho. Kwa wanaoujua wimbo hit wa Beyonce, Party yule anayerap sasa ndio J Cole mwenyewe.

Can’t Get Enough, Nobody’s Perfect na  Work Outbut ndizo nyimbo alizochagua kuziimba kesho katika shoo hiyo ya ufunguzi.



Habari kutoka: Mwananchi na Julieth Kulangwa  
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger