Hii ni familia ilionusurika kuteketea kwa moto baada ya jamaa kuwafungia wote ndani ya nyumba na kisha kuichoma nyumba moto usiku wa s Aprili 14 mwaka huu katika Kitongoji cha Mpakani, Kata ya Nsongwi Mantanji, Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. Familia hio ya watu sita ilinusurika usiku huo baada ya majirani kushuhudia Sakata hilo lilitokea baada ya kijana aitwaye Benard Andeson (25), ambaye ni jirani wa familia hiyo alipokwenda katika nyumba hiyo na kufunga kufuli milango ya nyumba hiyo, huku wakiwa wamelala; kisha kuichoma kwa moto na kutokomea kusiko julikana usiku huo. Wakati wa tukio hilo baba wa familia hakuwepo nyumbani hapo, ambaye anafahamika kwa jina la Bwana Japhet Mwalizi (55), ambaye yupo Nchi ya Malawi akitafuta riziki. |
Kwa habari zaidi bofya hapa:chimbukoletu.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment