Home »
» UUWWII MAJANGA: MAFUTA YA UBUYU SIO SALAMA KAMA YANAVYOSEMEKANA
UUWWII MAJANGA: MAFUTA YA UBUYU SIO SALAMA KAMA YANAVYOSEMEKANA
Mafuta ya Ubuyu ambayo yamejitwalia umaarufu siku za karibuni kiasi cha kufanya yawe ya bei mbaya sana yameelezwa kuwa si salama kwa afya..
TFDA wamepiga marufuku kwa kuwa yana Tindikali ya mafuta, na anayekunywa kwa wingi ana hatari ya kupata Kansa za aina mbali mbali. TDFA inaonya jamii kuwa mafuta hayo si mazuri na si salama na inashauri watanzania kuacha kutumia.
HABARI KAMILI HII HAPA KUTOKA HABARI LEO
Imechapishwa Jumatatu, 08 Julai 2013 | Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko
BAADA ya kuonya wananchi wanaotumia dawa za tiba mbadala ambazo hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), sasa inawataka wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa kama dawa.
Akizungumza na gazeti hili juzi katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana tindikali ya mafuta.
Alifafanua katika maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini kupata saratani za aina tofauti tofauti.
“Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wajasiriamali wanaouza mafuta ya ubuyu kama dawa, kwa kuwaelekeza wananchi kunywa. Napenda kuwataarifu kuwa mafuta hayo ni hatari kwani yana tindikali ya mafuta,” alisema.
Sos: Habari Leo..
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment