Na  Ezekiel
Kamanga Mbarali 
Mwanamke
aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani
kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya
amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja
baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka
miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za
kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba
nyingine  ya kuweza kuishi.
Mjane huyo
ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha
masika  ambapo baadhi ya vitu
vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa
kulala 
 “Mume
 wangu alifariki mwaka 2007 na  kuanzia mwaka 2010  serikali ya kijiji 
imenihamisha  na kunileta hapa bila huduma  za msingi  kama maliwato na 
bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri
kwa majirani  na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza
“ alisema mjane huyo.
 Kwa upande wake jirani wa mjane huyo  Bwana Mbwiga Mwayila amesema  kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha
hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na
hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa  adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .
 Bi  Salome
Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia
haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema  ameshuhudia 
mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba
anayoishi kuvuja na moto kuzimika 
 Naye  mwenyekiti
wa kijiji  hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwana  Fulugence  Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane
huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji  ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya
kulipa fidia  ingawa diwani huyo
hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .
0 comments:
Post a Comment