Akisimulia kisa anasema yeye na huyo aliyekuwa mume wake wamekuwa na mvutano juu ya hiyo nyumba.Alioana na mumewe mwaka 1998 na kuhamia katika hiyo nyumba mwaka 2000.Mwaka 2007 ndio migogoro ilipoanza baada ya mwanaume kuanza kutokurudi nyumbani na hatimae kutokurudi kabisa.Katika ndoa hiyo wana watoto watatu.Kwa muda wote mume amekuwa akitaka kumtupa nje na watoto wa kigezo kuwa hiyo nyumba sio yake mwenyewe anaitaka.Siku ya tukio jana yake mume alikuja akawachukua watoto akisema anaenda kuwanunulia vifaa vya shule hakuwarudisha.Asubuhi mama anashangaa watu wanaruka ukuta na kuvunja milango kumbe wamekuja mabaunsa na polisi kuwatupa nje.
Tukio la kushangaza lilitokea mitaa ya Sinza wakati mama huyu alipotupiwa vitu vyake nje ya nyumba baada ya kuvamiwa na mabaunsa chini ya usimamizi wa polisi. Mama huyu alisema mtu aliyemfanyia yote haya ni aliyekuwa mume wake na baba wa watoto wake.
Mwandishi wa habari hii na majirani waliokua eneo la tukio walijaribu kusaidia na kumpigia kamanda wa polisi kanda ya Kinondoni na mkuu wa kituo cha polisi osterbay ambako polisi walitoka huko kusimamia zoezi la kuhamishwa mama huyu, walipofanikiwa kuongea na mkuu huyo waliambiwa wao walipata barua kutoka mahakamani kuwa wanahitajika kusimamia ulinzi wakati mpangaji wa nyumba hiyo akitolewa nje. Mwanasheria wa huyo mama anasema wana kesi mahakamani kati yake na huyo mume ambayo haijaisha na inatarajiwa kusikilizwa kwa mara ingine tarehe 2 mwezi ujao.Na mbaya zaidi yeye hajapewa taarifa kuwa ahame ila amevamiwa.
katikati nyuma hapo pichani ni mama wa mwanamke huyu alietolewa vitu ndani, muda wote amekua akikaa na majirani wakimfariji bibi huyo baana ya kuonekana mwenye huzuni na mawazo mengi kwa muda wote alikua kimya na majirani wadai bibi aligoma kabisa hata kula...Majirani walikua na jazba na mabausa waliokuja kufanya tendo hilo la kinyama katika familia hii.
bibi pichani(hapo nyuma) ni mama wa huyu dada alietolewa nje, bibi alikua na hasira nyingi sana.
Jioni majirani ilibidi wamsaidie mwanamke mwenzao na kubeba vitu vyake na kuvihifadhi majumbani kwao kwa muda mpaka itakapojulikana hatma ya mama huyo.
majirani wakienda kuhifadhi vitu vya mama huyo kwenye nyumba zao..Na ilipofika usiku majirani walifanya fujo sana kiasi cha mapolisi kuingilia kati...ishu ilikuwa huyo anaedai ndio mwenye nyumba ajitokeze basi. Diwani wa eneo hilo nae ilibidi aje, ilibidi mapolisi pia waje kuwatoa hao mabaunsa na mama wa watu kurudishwa ndani ya nyumba yake usiku huo.
Kesho yake huyu mama aliamkia mahakamani na mahakama kuamua akae kwenye hiyo nyumba bila kubugudhiwa mpaka kesi yao itakapoisha.
Habari na Dina Marios
1 comments:
Maskini mama wa watu. wanaume wanyama jamani? ooiih, hapo ukute kapata dogo dogo sasa...
Post a Comment