DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh 200,000
Brandy
Nelson, Mbeya
DAKTARI wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Paul Ngiga
amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kushawishi na
kupokea Rushwa ya sh. 200,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa.
Akisoma
mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa Mbeya Francis Keshenye
Nimrodi Mafwele akishirikiana na Joseph
Mulebya alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa Desemba 19,2012 katika bar ya Victory.
Alisema kuwa
mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili moja likiwa ni la kufanya ushawishi na
la pili ni kupokea rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa ndugu wa mgonjwa ambapo
Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa
ilipoweka mtego wake na kufanikiwa kumkamata.
Ilidaiwa na mwendesha mashaitaka huyo kuwa mnamo desemba 18,2012 mshitakiwa aliomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa
ndugu wa mgonjwa aliyefahamika kwa jina la Meshack Mwakilambo kwa ni ya
kumsaidia kumhudumia mgonjwa wake.
Mwendesha mashitaka Mafwele
alisema kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria kanuni ya adhabu cha makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho
mwaka 2007 ambapo ni kifungu cha 15
kifungu kidogo cha kwanza (a).
Hakimu wa
mahakama ya haklimu mkazi Mkoa wa Mbeya Francis Keshenyi alisema mahamani kuwa
dhamana ipo wazi na kwamba kesi hiyo italetwa mahakamani hapo hadi
Desemba,27,2012.
Mshitakiwa
baada ya kusisomewa mashitaka hayo alikanusha kutenda kosa hilo na mshitakiwa
yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana na alidhaminiwa na mdhamini mmoja kwa gharama
ya sh 500,000.
0 comments:
Post a Comment