KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyetambulika kama Jenista Mapunda
(24) mkazi wa Mfaranyaki mjini Songea amejifungua mtoto kisha kumnyonga
na kumzika yeye mwenyewe alfajiri ya siku ya Jumapili (jana) katika
makaburi ya Mfaranyaki.
Watu
waliofika kushuhudia tukio hilo la aina yake walimshangaa kwa kuwa na
roho ya ukatili hali ambayo pia ilimfanya kuchimba kaburi yeye mwenyewe,
kumzika mwanawe na kuweka msalaba wa mti kama ilivyo desturi kwenye
maziko.
Kaburi
ambalo lilichimbwa na Jenista Mapunda(24) ambalo alimzika mtoto wake
baada ya kujifungua kisha kumzika na kuweka msalaba yeye mwenyewe
Kalista Kifaru(38) mkazi wa Mfaranyaki aliifahamisha FikraPevu kuwa
majira ya saa 12 alfajiri aliambiwa na mtoto wake ambaye alipita eneo
la makuburi kwamba amemuona mwanamke analia amelala juu ya kaburi ndipo
alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Mfaranyaki ndugu Gabriel
Ndewele.
Mwenyekiti
huyo wa mtaa akiwa pamoja na baadhi ya wakazi wa Mfaranyaki walikwenda
katika eneo la tukio ambapo walimkuta Jenista akiwa ameishiwa nguvu
kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Alipohojiwa
Jenista alidai kuwa ni kutokana na ugumu wa maisha ndiko kulimpelekea
alipojifungua karibu na vyoo vya shule ya msingi Misufini kuamua
kumnyonga mtoto wake hadi kufa kisha kumbeba na kwenda kuchimba kaburi
na kumzika kwenye makaburi ya Mfaranyaki.
Jenista
Mapunda(24) akiwa katikati ya polisi wawili ambao walimkamata baada ya
kudaiwa kumzaa mtoto, kumnyonga kisha kumzika yeye mwenyewe katika
makaburi ya Mfaranyaki mjini Songea
“Nilipojifungua
niliamua kumnyonga kubeba maiti kuchimba kaburi mimi mwenyewe kisha
kumzika, nilizidiwa peke yangu niliishiwa nguvu kutokana na kutokwa na
damu nyingi, niliamua kulia na kulala juu ya kaburi la mtoto wangu”,
alisema.
Polisi
wakiwa katika makaburi ya Mfaranyaki mjini Songea kufuatilia tukio la
Jenista Mapunda kudaiwa kumnyonga mtoto wake na kumzika
Polisi
wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo ambapo hivi sasa wanamshikilia
mwanamke huyo kwa upelelezi na uchunguzi zaidi. Hata hivyo mwanamke huyo
amepelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma na hali
yake inaendelea vizuri.
Habari hii imeandikwa na Albano Midelo, FikraPevu – Songea
0 comments:
Post a Comment