
Msanii
 Barnaba Elias ambaye anajulikana kwa sasa kama Baba Steve amekumbwa na 
maswahibu mfululizo ambayo itambidi kuwa makini la sivyo na yeye 
ataingia kwenye vitabu vya wasanii ambao wanakumbwa na mikasa inayoweza 
kumpelekea kukosa mwelekeo wa kimuziki.
 Kwa
 mujibu wa habari ambazo zipo kitaani msanii huyo alikumbwa na mkasa wa 
kwanza siku ya Jumapili iliyopita katika klabu ya usiku ya Club 
Billicanas ambapo wakati anatumbuiza kukatokea tukio la kusikitisha 
lililopelekea mpenzi wake, ambaye anajulikana kama Mama Steve kuswekwa 
lupango kwa kumpiga chupa msichana ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wa 
zamani wa Barnaba aliyekuwa akionyesha ishara za wazi wazi za kimapenzi.
Kwa
 mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari vilivyokuwepo katika Club hiyo 
ya usiku, baada ya kuona hivyo, Mama Steve alichukua chupa na kumpiga 
nayo msichana huyo ambaye alipasuka vibaya usoni na kuwahishwa polisi na
 kisha hospitali ili kupata matibabu, na kisha Mama steve ambaye ndiye 
mpenzi wa Barnaba kupelekwa katika kituo cha polisi Oysterbay ambapo 
inasemekana kuna maridhiano kati ya pande zote tatu na kila kitu 
kinakwenda sawa.akiongea nakipindi cha xxl cha clauds fm Barnaba 
alidhibitisha kutokea tukio hilo
Baada
 ya tukio hilo, inadaiwa kuwa kuna msichana mwingine anayeishi maeneo ya
 Mwananyamala wilaya ya Kinondoni ambaye anamtafuta Barnaba ili ambwagie
 mtoto kwakuwa anadai amekuwa hampi sapoti yoyote katika matunzo.
Binti
 huyo, inavyosemekana anatafuta nafasi ambapo msanii huyo atakuwa na 
shoo na yeye atatafuta upenyo wa kwenda kumbwagia mtoto huyo!!
Tunachojaribu
 kujiuliza hatujui ni mdudu gani aliyeingia katika tasnia ya muziki wa 
kizazi kipya husasan Bongo Flava kwakuwa ‘trends’ za sasa zinaonyesha 
matukio yasiyo ya kawaida kwa wasanii wetu yameendelea kushika kasi na 
hili la Barnaba ni moja ya vitu vinavyotufanya tujiulize, je! kama 
itatokea hivyo mambo hayo hayawezi kupoteza focus ya msanii? Au wasanii 
wanaoonekana kukomaa na hivyo kuzima nyota zao za kisanii wakiwa bado 
hawajadumu vya kutosha?
Kwa hisani ya http://dj-sek.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment