Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.
Wakipiga picha na baadhi ya watalii waliowakuta hapo.

Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakiwa katika picha ya pamoja, jana wakati warembo hao walipo tembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuopata maelezo na kuzungumza na watalii na wapanda mlima huo. Warembo 29 na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani.
Mbali na kutembelea hifadhi hiyo lakini warembo hao walishiriki katika tamasha la michezo kwa ajili ya kuchangia fedha na vitu mbalimbali vya watoto Yatima vya jijini Arusha.
Picha kwa hisani ya : http://www.sufianimafoto.blogspot.com/
1 comments:
mmh warembo natafuta mchumba hapo vipi nitapata au wote mshachukuliwa?
Post a Comment