Home » » REDD'S MISS TALENT 2012 HUYU HAPA

REDD'S MISS TALENT 2012 HUYU HAPA


  
Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya Redd's Talent iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Gireffe,jijini Dar es salaam.Kutoka kulia niMshiriki namba 13 kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi,Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana,Mshiriki kutoka Kanda ya Mashariki,Irene Verda na Mshiriki namba 26 kutoka Kinondoni,Brigit Alfred.
 Mgeni Rasmi katika Onyesho la Redd's Miss Talent,Mbunge wa Viti Maalum - Arusha,Mh. Catherine Magige (katikati) akizungumza machache wakati akifungua shoo hiyo iliyofanyika hivi sasa katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Bekon.
                       
Babylove Kalala akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili kwa kutimia Nyoka.( Huyu ndiye alienyakua Taji la Redds Miss Talent wa mwaka huu) 
 Mshiriki namba 11 kutoka Kilimanjaro,Nandi Rafael akionyesha umahiri wake wa kusakata dansi.
 weweee hapana chezeya mshiriki namba 29,kutoka Dodoma,Belinda Mbogo nae akisakata Dansi.
 Mrembo kutoka Chuo Kikuu Huria, Zuwena Naseeb akionyesha umahiri wake wa kuimba katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
 Mrembo kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi akionyesha uwezo wake wa kuyarudi mangoma
 Mrembo huyu ni mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Michael akionyesha kipaji chake cha kuimba.
 uuwwiii chezeya watu na mazoezi kudadaddddeeee iga msamba huo uchemshe lol, huyu ni mshiriki namba 8 kutoka Kanda ya Ziwa,Happyness Rweyemamu akionyesha kipaji chake cha kuruka sarakas
 Mrembo aliokua na  namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana akionyesha kipaji chake cha kupiga Zeze.
Mshiriki namba 7 kutoka Rukwa,Vency Edward akionyesha kipaji alichonacho cha kucheza.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger