Home » » PICHA TANO ZA TUKIO LA MWANAFUNZI NA MTU MZIMA KUJINYONGA MKOANI MBEYA

PICHA TANO ZA TUKIO LA MWANAFUNZI NA MTU MZIMA KUJINYONGA MKOANI MBEYA

 Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao. Chanzo cha mtoto huyo kujinyonga hakijajulikana bado
 Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8)
 Mama mzazi wa marehemu Kervin Patrick (8)Bi Subira Patrick(38) akiwa katika hali ya majonzi kufuatika kifo cha mwanae aliyejinyonga.
WAKATI HUO HUO: Baadhi ya mashuhuda walikutwa wamekusanyika kushuhudia Mwili wa Mkazi (mtu mzima tu) wa Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55)  amejinyonga kwa kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho. Pia na huyu mpaka tunaruka hewani kisa chake yeye kujitoa uhai kwa kujinyonga hakikujulikana
Mke wa marehemu Mbwiga Bi Malita Mbwiga(45) wa pili kutoka kulia akiwa na baadhi ya akina mama waliofika kumfariji kufuatia kifo cha mumewe(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya)

Habari kwa hisani ya CHIMBUKO LETU. blogspot.com
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger