Home » » KAMANDA WA POLISI MKOANI MWANZA LIBERATUS BARLOW AMEUAWA KWA KUPIWA RISASI

KAMANDA WA POLISI MKOANI MWANZA LIBERATUS BARLOW AMEUAWA KWA KUPIWA RISASI



Mkuu  wa  jeshi la  polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha  kuuwawa kwa kakamnda  wa  Mwanza Liberatus Barlow .


Amesema  kuwa  kamanda  huyo wa polisi ameuwawa na  watu  wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30  na saa 8 usiku   katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Mwema amesema  kuwa kamanda  Barlow alikuwa akitokea katika  kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla  alikutwa na tukio  hilo la  kupigwa  risasi.

Hata  hivyo alisema  kuwa  kutokana na tukio  hilo jeshi la  polisi  linatarajia kuanza uchunguzi  wake kuanzia leo na timu ya askari  kutoka  makao makuu ya polisi  wataondoka mapema leo kwenda  jijini Mwanza  kuungana na askari wa mkoa  huo kwa ajili ya uchunguzi  zaidi na msako wa majambazi hayo .

Mwema amewataka  wananchi  wa Mwanza  kutoa ushirikiano wao kwa  jeshi la polisi ili kufanikisha  zoezi hilo na  kuwataka kutokuwa na hofu  yoyote kutokana na tukio  hilo.

NEWS UPDATE: NYUMBANI KWA MAREHEMU
Mtoto wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo aliposikia risasi ikipigwa.
Ndugu jamaa na marafiki wakiendelea kuomboleza nyumbani kwa marehemu Barlow

Ndugu na jamaa wa marehemu Barlow....

picha na http://wotepamoja.com/
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger