Home » » VIPODOZI HATARISHI VYAZIDI KUSAMBAA MOSHI

VIPODOZI HATARISHI VYAZIDI KUSAMBAA MOSHI



WAKATI Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),  ikipiga marufuku matumizi ya vipodozi hatari kwa afya za binadamu, vipodozi hivyo sasa vimetapakaa katika maduka mbalimbali ya vipodozi mkoani Kilimanjaro.

Hali ni mbaya zaidi katika mji wa Moshi na vitongoji vyake ambapo baadhi ya Maofisa wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamegeuza biashara hiyo kuwa mradi ambapo ‘humalizana’ kiaina na wamiliki wa maduka hayo.
 
Uchunguzi wa gazeti la Mwananchi ulibaini baadhi ya maduka hayo kuuza  vipodozi hivyo kwa usiri mkubwa kwa kutazama sura ya mteja ambapo sehemu kubwa ya wale wanaouziwa ni wanawake  huku wanaume wakitiliwa mashaka. Vipodozi vilivyozagaa kwa wingi ni Carolight, Mekako, Maxi Light, Bio Carote, Carottene na G&G cream, Rico Cream, Princes Cream na Clare Cream ambavyo TFDA ilitangaza vipodozi hivyo kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.

Maduka yaliyosheheni vipodozi hivyo yapo katika stendi kuu ya mabasi Moshi Mjini, stendi ya Soweto, Barabara ya Nyerere maarufu kama Double Road, maeneo ya KCMC na baadhi ya maduka ya bidhaa za rejareja yaliyopo kwenye makazi ya watu.

Katika kuthibitisha kuzagaa kwa vipodozi hivyo, mwandishi wa habari hizi aliamua kumkodi  mwanamke mmoja na kuzunguka naye katika maduka sita kununua vipodozi hivyo na akauziwa japo vilikuwa vikichukuliwa nje ya makabati ya bidhaa.

Habari zaidi zilidai kuwa Afisa mmoja wa Afya katika Manispaa ya Moshi(jina tunalo) amekuwa akipita katika maduka hayo mara moja au mbili kwa mwezi na kuchukua hongo ya kati ya sh100,000 na sh200,000 kwa kila duka.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Dk. Christopher Mtamakaya alipoulizwa jana alisema hana taarifa juu ya kuzagaa kwa vipodozi hivyo na kuahidi kufanya operesheni ya kukagua maduka yote ya vipodozi.

Tayari TFDA ilishatoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa vipodozi karibu 200 ambavyo vimetengenezwa kwa madini hatari ya Hydroquinine, Steroids, Bithionol na Zebaki ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu.
Taarifa hiyo ya TFDA inasema vipodozi hivyo hatari huweza kusababisha kansa ya ngozi kwa mtumiaji, akina mama kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na uharibifu wa ini na figo na athari huchukua muda mrefu kutambuliwa.



Haya habari hio nimeitoa gazeti la Mwananchi.....Ila sasa mi najiuliza kama mnajua vipodozi hivi vinamadhara kwanini wanaruhusu viingie nchini in the first place? Sasa mnakataza vipi watu wasivitumie ilhali mmeruhusu makontena kwa makontena ya hivyo vipodozi yaingie? mweeeh 

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Sweet Home - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger