Sherehe, nderemo na vifijo katika Ukumbi wa Mikutano, mara baada Mheshimiwa Jaji Munuo kutangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Chama hicho na Tanzania kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano ujao wa Chama hicho Mwaka 2014.
Chama cha Majaji Wanawake duniani (IAWJ) kilikuwa na mkutano wake Mkuu uliofanyika London Uingereza tarehe 2-5 Mei 2012.
Kwenye Mkutano huo Tanzania, iliwakilishwa na Majaji na Mahakimu ambao ni wanachama wa IAWJ (International Association of Women Judges) na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA).
Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali walichaguliwa kushika nyadhifa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili.
Mhe. Jaji Eusebia Munuo, ambae pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.
Pamoja na kuchaguliwa ktk nafasi hiyo,Mheshimiwa Jaji Munuo, pia alikabidhiwa rasmi Bango la chama hicho. Kwa kukadhiwa Bango hilo, Tanzania sasa imekabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkuu ujao wa chama hicho. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Arusha Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania uliokuwepo kwenye mkutano huo ulipokea wadhifa huo kwa shangwe na furaha kubwa kama inavyonekana kwenye picha.
Tanzania itashikilia nafasi hiyo ya Urais wa chama hicho mpaka mwaka 2014.
Habari na picha kwa hisani ya: http://magangaone.blogspot.com/
Home »
»
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:
Post a Comment